Karibuni swahilivilla blog,Blog hii imeanzishwa mjini Washington Dc na inaendeleza kazi zake katika mji wa Maryland. Inatumia lugha ya kiswahili na kingereza ili kuhabarisha kuhusu maswala mbalimbali ya kijamii hasa katika ukanda wa Marekani mashariki na Afrika mashariki. Itakuwa inakuletea habari mbalimbali za kijamii, siasa, burudani,michezo nk. Nakaribisha maoni yenu. Wasiliana nasi kwa namba ya Simu {301}728-3977 Email:kijiko12@hotmail.com.

Wadau wa facebook

Saturday, May 19, 2012

UNYWAJI POMBE WA MWANAFUNZI AWAPO DARASANI WAMSABABISHIA KUFUKUZWA SHULE MKOANI MBEYA.

Na Pulkeria Kisoka, Mbozi.

Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Mlowo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Tabu Mfyeti, amefukuzwa shule baada ya kukutwa akinywa pombe darasani na wengine 9 wakiwa kwenye uchunguzi na maamuzi ya bodi.

Akiongea na mwandishi wetu Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Sufyan Msarilwa, amesema mwanafunzi huyo ni wa kike na alikutwa akinywa pombe na amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara wakati wa masomo pamoja na wenzake hao 9 ambao wanaendelea kuchunguzwa.

Kwa upande wake mwanafunzi huyo Tabu amekiri kutenda kosa hilo na kwamba amekuwa akinywa pombe kwa madai ya kuwa hawezi kusoma bila kufanya hivyo.

Hata hivyo jitihada za wazazi wa mwanafunzi huyo kuuomba uongozi wa shule hiyo kumsamehe mtoto wao zimegonga mwamba kutokana na kile kilichotamkwa na uongozi huo kuwa wamechoshwa na tabia chafu za mwanafunzi huyo.

Friday, May 18, 2012

Sikiliza kwa makini hutba ya leo Ijumaa May 18,2012 iliotolewa na, Imam Azad Ali, Avondale Islamic Center, 4637 Eastern Avenue, Mount Rainier

Chalsea ya tua Munich kwa mechi ya kesho dhidi ya Bayern Munich

Here we go: Chelsea players (from left) David Luiz, Didier Drogba and Ramires preparing to fly out to Munich
Haya tena kama kaweaida wachezaji wa Chelsea wakijianda kwa safari ya  Munich nchini Germarn (kutoka kushoto) David Luiz, Didier Drogba katika mchezo wa Final ya mchezo Champions League kesho na  wa Bayern

Touching down: Didier Drogba steps off the plane with the Chelsea squad in Munich
Safari na kuziki wameruka na wametua kwea usalama, Didier Drogba akionekana kushuka ndani ya ndege na majeshi yake kikamilifu ndani ya Munich leo hii

Let's go! Raul Meireles, Michael Essien, Florent Malouda and John Obi Mikel leave the plane Majeshi mbele mchezaji Raul Meireles, Michael Essien, Florent Malouda na John Obi Mikel wakishika ndani ya ndege

Leaders: John Terry and Frank Lampard walk off the plane
Kiongozi: John Terry naFrank Lampard wakitoka ndani ya ndege

I recognise the hair, sir: David Luiz has his passport checked by police at the airport
Mzushi Polisi akiangalia Passpart ya ukiona nyele tu umeshapata jibu, David Luiz

Kwa wale wapenzi wote wa timu ya Chelsea tupo pamoja maneno kesho furaha au kutokua na furaha pale Refa atakapopuliza penga ya mwisho, kila la kheri.

UTIAJI SAINI WIZARA YA MIUNDO MBINU ZANZIBAR‏

Na Talib Ussi Zanzibar

ZAIDI ya b65 Tsh. Zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho na utanuzi wa njia za kurukia na kutua ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Zanzibar unaojuilikana ‘Abeid Amani Karume International Airport.’

Hayo yameelezwa katika hafla ya utiaji saini kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya SOGEA kutoka Ufaransa katika Ofisi za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Malindi mjini Zanzibar.

Katika hafla hiyo katibu Mkuu wa Wizara hiyo Vuai Haji Lila alitia saini kwa niaba ya SMZ na Laurent Brouet ambaye ni msaidizi wa Meneja wa kampuni hiyo kwa kanda Afrika ya Mashariki ndiye aliyeweka saini kwa niaba ya kapuni yake.

Akifafanua juu ya utiaji saini huo Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Ussi alisema pesa hizo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (IDA) ambazo ziliombwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Naibu Waziri huyo alifahamisha kwamba kutekeleza ujenzi huo ni kutimiza mikakati ya Serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi na kuongeza uingiaji wa Watalii humu nchini.

Alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutapelekea Ndege nyingi kuingia Zanzibar na wageni kupata nafasi ya kutembelea Nchini jambo ambalo litachochea maendeleo.

“Viwanja vya Ndege ndivyo vinavyotumika sana kwa kuingiza watalii na uwanja wetu ukikamilika tunatarajia kupokea watalii wengi”alisema Ussi ambaye ni Naibu Waziri.

Ussi alisema mbali na kuongezeka Shughuli za Utalii bali na Wananchi wataweza kupata ajira nyingi tokea mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika na pale utakapoanza kutoa huduma.

Facebook Mida Ya Kazi

WANA DIASPORA FIKA TUJADILI MAENDELEO YA NCHI WASHINGTON DC

swahilivilla.blogspot.com

MAZISHI YA MAREHEMU PATRICK MAFISANGO

  
Mwili wa marehemu Partrick Mafisango ukiwasili vianjwa yva TCC mapema leo. (Picha ya Pili Kulia) Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa, Juma Nyoso (kushoto) na John Boko, wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mafisango kuupeleka sehemu iliyopangwa.

Jeneza likiwa na kombe la ubigwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania lililotwaliwa na Simba mwaka huu.

Kutoka kushoto ni msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga, Kocha wa Simba Milovan Cirkovic na goalkeeper wa Simba Juma Kaseja wakilia kwa uchungu

Baadhi ya waombolezaji msibani hapo . Mwili wa Marehemu kwa sasa uko njiani kuelekea nyumbani kwao, Kinshasa Congo ambako ndipo atakapo zikwa.

Blog hii inapenda kutoa pole kwa Club ya Simba, wapenzi wote wa michezo na familia ya marehemu.

Na picha zote kwa hisani ya Globalpublishers
Kupitia kwa Jestina George




Donna Summers Afariki Dunia akiwa na Umri wa Miaka 63!

Mwana muziki maarufu kwa miaondoko ya soul train malkia Donna Summer alifariki asubuhi hii baada ya kuungua na ugonjwa wa Saratani. Blog ya swahilivilla ina heshima kubwa kwa kifo cha mwana muzikia huyo kufuatilia rekodi zake.

Labda tukuchezee moja ya kibao chake Maarufu kinachoitwa "Last Dance" nadhani mdau utakuwa unakikumbuka katika miaka ya 1978 R.I.P Donna Summey

Mkutano wa kilele wa G8 kuanza Camp Dave

Am Randes des G8-Gipfels in Washington haben sich die Außenminister der USA und Russlands, Clinton und Lawrow (links) auch zu bilateralen Konsultationen getroffen. - US Secretary of State Hillary Clinton (R) and Russian Foreign Minister Sergei Lavrov (L) prepare to hold a bilateral meeting at Blair House in Washington DC, April 12, 2012. The officials are wrapping up two days of talks during the G-8 Foreign Ministers Meetings. REUTERS/Mike Theiler (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
eingestellt von: ml
Rais wa Marekani Baracka Obama anamkaribisha leo katika ikulu ya White House Rais mpya wa Ufaransa, Francois Hollande kabla ya viongozi hao wawili kujiunga na wenzao katika mkutano wa kilele wa nchi tajiri ulimwenguni G8

Rais Obama analenga kuimarisha uhusiano wa Marekani na Ufaransa na kisha kisha kuishinikiza Ulaya kujitahidi zaidi katika kutatua mgogoro wa kiuchumi unaoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Francois Hollande, aliyeapishwa mapema wiki hii kama rais mpya wa Ufaransa, tayari ameibua hisia kali kwa kupinga mpango wa Ulaya wa kubana matumizi na kusema kuwa ataviondoa vikosi vya Ufaransa kutoka Afghanistan ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Obama kumhimiza Hollande

Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutano unaopangwa kuanza Camp Dave
Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutanowa 
kilele unaopangwa kuanza Camp Dave
Obama mwenye umri wa miaka 50 huenda akautumia mkutano wake wa utangulizi katika ofisi yake kumhimiza Hollande mwenye umri wa miaka 57, Msoshalisti kutathmini upya mipango yake ya Aghanistan ambayo imeiweka Ufaransa katika ratiba ya kuondoka nchini humo mapema kuliko washirika wake wengine wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Lakini viongozi hao wawili ambao wameleezea uungaji mkono wao kwa sera za ukuaji wa kiuchumi barani Ulaya, wanatarajiwa kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo wa madeni unaoukumba ukanda unaotumia sarafu ya euro, ambao huenda ukaugubika mkutano wa mwishoni mwa wiki wa kundi la nchi nane tahiri zaidi ulimwenguni.

Utawala wa Obama ulitumia fedha nyingi kupambana na mdororo wa uchumi wa mwaka wa 2007-2009, na Hollande analenga kuutumua mpango wa kubana matumizi kwa kupitia uwekezaji wa kubuni nafasi zaidi za ajira.

Mkutano wa kilele wa G8 unajiri wakati Wagiriki wakiendelea kuondoa pesa kwenye akaunti zao kutokana na kuongezeka hofu kwua nchi hiyo itaondoka katika kanda ya sarafu ya euro, na masoko ya hisa yameingiwa hofu kuhusu uwezekano wa kuibuka mgogoro mkubwa wa kiuchumi ulaya.
Mzozo wa Ugiriki wazua hofu

DK..Shein Akutana na watendaji wa Wizara ya Habari Utamanduni Utalii na Michezo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,utamaduni na Michezo,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar jana,(kushoto) Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.

Baadhi ya Wakurugenzi na Maofisa wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Habari wakiwa katika mkutano na Rais wa Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika kujadili utendaji wakazi kwa kipindi cha miezi mitatu kwa Wizara hiyo,ukiwa ni mpango wa Rais wa kuzungumza na kila Wizara,mkutano huo ulifanyika jana Ikulu Mjini Unguja.

Kwa picha zaidi tembeleah othmanmapara.blogspot.com/

US, Africa for stronger trade ties

The US Assistant Secretary of African Affairs, Johnnie Carson

By JAFFAR MJASIRI

Africa and the United States will continue to be trading partners, the US Assistant Secretary of African Affairs, Johnnie Carson, has said.

Carson said as a gesture of significant partnership with Africa in trade and many other areas, President Barrack Obama has invited President Jakaya Kikwete and three other African leaders to attend the 38th G-8 Summit, at Camp David, Maryland, today and tomorrow.

The US Assistant Secretary of State was talking to journalists from various African cities during a tele-conference late Wednesday.

President Kikwete, African Union Chairman, who is also Benin President, Yayi Boni, Ghana’s John Mills and Ethiopian Prime Minister Meles Zenawi would join leaders of the group of the world’s richest nations at the summit. The G-8 group comprises the US, Britain, Japan, France, Germany, Italy, Canada and Russia.

Mr Carson said the US president’s Feed the Future project which focuses on agriculture will feature at the Summit. He said President Obama will speak at the Summit on food security, agriculture and food self-sufficiency.

In Kenya: Saitoti on the spot over county appointments

Upo umuhimu mkubwa wa kuongeza ushirikiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamuhuri ya Cuba. "Balozi Seif "

Na Othman Khamis Ame

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema upo umuhimu mkubwa wa kuongeza ushirikiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamuhuri ya Cuba hasa katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kwa nia ya kustawisha Uchumi wa Pande hizo mbili.

Balozi Seif alitoa wazo hilo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Biashara za Nje na Uwekezaji vitega uchumi wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Rodrigo Malmierca Diaz yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mjini Havana Nchini Cuba.

Alisema Maendeleo makubwa na ya haraka yanaweza kupatikana katika kipindi kifupi iwapo pande hizo mbili zitafikia maamuzi ya pamoja katika kuzishirikisha Sekta binafsi kwenye Mpango huo muhimu wa Uchumi.

Alisema Tanzania na Zanzibar kwa ujumla tayari zimeshafungua milango kwa Taasisi Binafsi za Biashara na Uwekezaji kutoka Nje ya Nchi na kupelekea hali ya Uchumi kukua hatua kwa hatua.

Balozi Seif aliishauri Cuba kuitumia fursa hiyo kwa kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya Nchi hiyo kuwekeza Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla kwa vile maeneo mengi bado yana rasilimali za kutosha katika uwekezaji Vitega Uchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea kuvutiwa kwake na Mfumo wa Utalii unaoendelezwa Nchini Cuba ambao umepelekea Nchi hiyo kukusanya Mapato mengi yatokanayo na Sekta hiyo.

WATU 6 WA FAMILIA MOJA WANUSURIKA KIFO BAADA YA MOTO KUZUKA.

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Watu 6 wa familia moja wamenusurika kifo baada ya moto kuzuka katika mtaa wa Ilolo, Kata ya Ruanda, Jijini Mbeya, Mei 17 mwaka huu.

Tukio hilo limetokea baada ya familia hiyo ya Bwana Ezekiel Mwasandube na mkewe Bi Christina Kyamba kulala na moto huo kuanzia sebuleni, ambapo inadaiwa kuwa dirisha la nyumba yao lilivunjwa na mtu au watu wasiofahamika kisha kuwasha moto kwa kutumia ufagio wa kupigia deki(mopu) ulionyunyiziwa mafuta ya taa na baadae kutokomea kusikojulikana.

Wengine walionusurika ni pamoja na Eva Mwasandube ambaye mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Sinde na Tabea Mwasandube ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Meta na William Mwasandube.

Wazazi walisikia yowe kutoka kwa watoto wao Eva na Tadea na walipojaribu kutoka kujua kulikoni ndipo wazazi walikumbana na wingu nzito la moshi ndipo waliomba msaada kwa majirani ambao walifika na kuvunja mlango na madirisha yaliyokuwa na vizuizi (grill) na kuwaokoa wanafamilia hao.

Veteran Algerian singer Warda passes away in Cairo at the age of 72

The Algerian singer Warda was well known for singing patriotic songs. (File photo)
The Algerian singer Warda was well known for singing patriotic songs. (File photo)

By AL ARABIYA

Veteran Algerian singer Warda passed away at the age of 72 at a hospital in the Egyptian capital Cairo, after a long singing career that extended for over half a century.

Her son Riyad Qasry confirmed the news to Al Arabiya and said that she will be buried in Algeria, upon the instructions of Algerian President Abdelaziz Bouteflika.

Warda was born in France in 1940 to a Lebanese mother and an Algerian father. She started her singing career at the age of 11. She quickly became well known for her singing of patriotic Algerian songs.

In 1972, Algerian president Houari Boumédienne asked her to sing to commemorate the country’s independence, and she performed with an Egyptian orchestra.

She then moved to Egypt, where she married the late composer Baligh Hamdi. They teamed up in many songs that added more to the fame of Warda.

In addition to singing many songs to other Arab composers, Warda starred in a string of successful movies.

Her last work was a video-clipped song marking the 50th anniversary of Algeria’s independence

Statesmen's Forum: President Kikwete of Tanzania

Please join us for a conversation between Tanzanian President Jakaya Kikwete and MCC Chief Executive Officer Daniel W. Yohannes.

Introduction by Jennifer Cooke Director, Africa Program, CSIS

Tanzania represents a success story for developing and emerging-market countries in a time of changing donor-recipient relations. Through a series of reforms to increase transparency, good governance, and country-led development, President Kikwete has helped Tanzania become a strong partner with the United States and the business community.

Tanzania is the recipient of a $698 million Millennium Challenge Corporation compact, hosts a robust PEPFAR program, launched the Southern Agricultural Growth Corridor (SAGCOT) initiative, and was among the first countries selected for the Partnership for Growth—all of which have helped Tanzania make gains in enhancing food security, reducing poverty, and creating economic opportunities.


Thursday, May 17, 2012
3:00 p.m. - 4:00 p.m. B1 Conference Center, CSIS 1800 K St. NW, Washington, DC 20006

Washington Musicians Remember Chuck Brown's Generosity