Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Saturday, August 21, 2010

Ramadhani 2010 Sala ya ijumaa Masjid (MCC) 15200 New Hampshire Ave Silver Spring, Maryland

Msikiti wa Mcc Uliokuwepo kwenye barabara ya New Hampshire Silver Spring katika mji wa Maryland nchini marekani.

Muhammed , Zuhura, na Muhanna wa kijipatia picha kabla ya sala ya ijumaa kuaza, wakiliaga kwa unyonge kumi la awali la rehema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kareem. 2010


Waumini wakisali sala za sunna kabla ya sala ya ijuma kuaza.

Baadhi ya waumini kukosa nafasi za ndani wakionekana wakisali njee yaeneo la msikiti huo.

Ndani ya msikiti wa Mcc New Hampshire silver Spring Md Waislamu wakisali sala za sunna kablia kabla yakusali salaa ya Ijumaa.


Waumini wa masjidi MCC New Hampshire katika mji wa maryland nchini marekani wakitoa michango ya kusaidia watu waliopata mafuriko katika nchi ya Pakistan iliyo tokea wiki iliyopita.

Kumi la mwanzola rehema, lishakwisha na tumeanza kufunga juzi tu sasa jiangalie ktk kumi hili umefanya jambo gani jeema la kumpendeza Allah na kama hujafanya, wakati wako ndio
huu. katika kumi la kuomba madhfura inshaAllah Ameen.

HEKO KUMI LA REHEMA

  1. Bismillahi ‘Aliyyun, Ya Ilahi Ya Rahimu
    Bismillahi Qawiyyun, nguvu ni Zako Qayyumu
    Bismillahi Ghafurun, toba ni Kwako Hakimu
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  2. Bismillahi Basirun, unatuona wajao
    Bismillahi Samiun, tusikize viumbeo
    Bismillahi Munirun, nawirisha wakuchao
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia

  3. Rehema Zako Rabana, zeleya kila mahala
    Rehema za Subhana, zenda kwa hata kabwela
    Rehema za Maulana, kwa ‘asi na mcha Mola
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  4. Awali ya Ramadhani, kumi limejaa heba
    Kwa kusoma Qur’ani, na kukithirisha toba
    Wokovu kwa waumini, Rabbi utupe haiba
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  5. Tufunge tukihimidi, rehema zako Rabbana
    Tufunge tukikunadi, turehemu Ewe Bwana
    Tufunge tukiburudi, Amina Rabbi Amina
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  6. Tukitaja jina Lako, tuburudike nafusi
    Tukiona waja Wako, tukukumbuke Mkwasi
    Tukiwa na Peke Yako, tujiepushe kuasi
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  7. Tukwogope hadharani, na zaidi faraghani
    Kubali wetu ugeni, Ilahi Ya Rahmani
    Bila ya Kwako Manani, twende kwa mwengine nani?
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

  8. Takabali zetu dua, saumu na sala pia
    Waja tumejaa doa, pumzi zinafifia
    Hatutendi kwa kujua, Ya Rabbi twakulilia
    Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

Ahmed Rashid.

No comments:

Post a Comment