Picha ya kwanza ni mfuasi wa CCM, Makala Joseph akionesha kitambaa kilichosababisha kupigwa na wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa TLP huko Himo, Moshi, Kilimanjaro. Inaripotiwa na Dixon Busagaga kuwa kijana huyo akiwa na kitambaa chake chenye nembo za CCM, alishuka toka kwenye gari eneo la Njia Panda ambapo mgombea Ubunge wa Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustino Mrema alikuwa akizindua tawi la chama eneo hilo; wafuasi wa TLP walipomwona na kitambaa hicho na walipotaka kumnyang'anya naye akionesha kutokukubaliana nao, ndipo wakaanza kumshambulia hadi kumjeruhi na kusababisha kufikishwa Zahanati kwa ajili ya matibabu ambapo alishonwa nyuzi kadhaa eneo la chini ya jicho alipojeruhiwa.
Watu wanasema Mrema huendesha kampeni mahala popote penye umati wa watu bila kufuata utaratibu unaoelekeza kuwepo na ulinzi wa askari mikutanoni. Endelea kusoma habari hii katika blogu ya Michuzi.
Watu wanasema Mrema huendesha kampeni mahala popote penye umati wa watu bila kufuata utaratibu unaoelekeza kuwepo na ulinzi wa askari mikutanoni. Endelea kusoma habari hii katika blogu ya Michuzi.
Picha ya pili ni Didi Msira Koko ambaye ni Mwenyekiti wa CUF wilayani Musoma Mjini na mgombea udiwani wa kata ya Iringo, ambaye alipigwa na kujeruhiwa vibaya na watu aliowataja kuwa ni wafuasi wa CCM jimbo la Musoma Mjini. Didi amelazwa katika hospitali ya Serikali ya Mkoa Mara na kufanyiwa uchunguzi zaidi. Alipatwa na mkasa huo baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete katika uwanja wa shule ya msingi Mukendo kuisha. Anasema, baada ya kumalizika mkutano, akiwa anaelekea maeneo ya Iringo, aliitwa na kundi la vijana ambao ni ndugu na wafuasi wa mgombea ubunge wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo, na kuanza kumuuliza juu ya sera za CCM.
Didi aliwajibu kuwa kila chama kina sera na mwananchi atasikia ni sera ya chama gani nzuri na kuamua kuipa kura, katika kujieleza na kufafanua hayo, anasema kijana mmoja kwa jina, Mapinduzi, alimvamia na kuanza kumpiga kwa kuwa anampinga Mathayo. Endelea kusoma habari hii katika blogu ya Mgendi.
Najiuliza...
Ni dhahiri kuwa mwendo huu si mzuri hata kidogo. Hii kupigana na kuumizana hivi huzua visasi ambavyo ugomvi wake waweza usiishe kimya kimya. Huko ndiko tunakotaka Watanzania kwenda hata baada ya kuyaona yaliyotokea kwa majirani zetu? Tunajifunza na kukumbuka ama tunataka tupite mumo humo? Kwani siasa zinapopishana, upo ulazima wa kujeruhiana wakati hatima ya yote i katika vituo vya kupitia kura? Twaishia kutwangana na kulemazana sisi tulio nguvu kazi ya Taifa, wenyewe viongozi wala hawamo! Mazuzu!

No comments:
Post a Comment