Msemo huo husemwa sana pale mtu anapokuwa amekosea kutamka neno au kutamka neno ambalo hakulimaanisha kwa wakati ule.
Msemo huu umemkuta mbunge wa Handeni Tanga Dk.Abdallah Kigoda baada ya bila kujifahamu alijikuta akimnadi aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Bw. Benjamin William Mkapa kwa kusema (Mkapa Oyeeee….!!!) badala ya mgombea urais wa sasa kupitia chama tawala CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Dk.Kigoda alikutwa na mahasibu hayo wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge kupitia chama hicho jimbo la Kilindi Bi. Beatrice Shelukindo zilizofanyika katika kijiji cha Kwediboma


No comments:
Post a Comment