If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, November 25, 2010

KULA ASALI NA MDALASINI KUPUNGUZA UNENE!


Karibuni tena katika sehemu ya pili ya makala yetu ya leo kuhusu kupunguza unene, mada ambayo imeonekana kuvuta hisia za wasomaji wengi. Tatizo la unene limekuwa sugu. Kila mmoja anajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hilo. Wiki iliyopita nilianza kuelezea uzito anaopaswa kuwa nao mtu kulingana na urefu wake.

Kwa kuzingatia maelezo yale, sina shaka sasa umeshajua unatakiwa kupunguza kilo ngapi. Ingawa kuna baadhi ya wasomaji wametaka kujua jinsi ya kuongeza uzito, lakini kwa leo hatutaweza kuzungumzia hilo, tutaandaa makala yake siku nyingine, kwa sababu ni vitu viwili ambavyo vinahitaji kuongelewa kwa upana. KANUNI ZA KUPUNGUZA UZITO Kanuni ya kwanza ya kupunguza uzito inatueleza kuwa ili mtu upunguze uzito, unahitaji kutoa kalori nyingi mwilini na kuingiza kalori kidogo (Less Calories In + More Calories Out= Weight Loss). Kwa lugha nyepesi, unapokula chakula chochote unaingiza kalori mwilini na unapofanya mazoezi au kazi yoyote unatoa kalori mwilini.

 Hivyo kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako. ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula. Matumizi ya asali ni rahisi sana.

Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya. Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali. Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.

 Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki. Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.

 ASALI NA MDALASINI Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku. Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka. Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.

1 comment:

  1. naomba toleo lililo pita nitalipata vipi kuhusiana na zito anaopaswa kuwa nao mtu kulingana na urefu wake.

    ReplyDelete

Maoni yako