Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Friday, December 31, 2010

NDANI YA KENYA RAIS KIBAKI ASAINI MISWAADA MITATU KUWA SHERIA NCHINI KENYA…!!!


Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametia saini kuwa sheria miswada mitatu itakayo wezesha kuundwa kwa kamisheni muhimu zitakazo chochea utekelezaji wa katiba mpya. 

Taarifa kutoka idara ya habari ya rais imesema rais Kibaki amesaini kuwa sheria miswada ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Utekelezaji wa Katiba, Kamisheni ya Mpangilio wa Mapato na Kamisheni ya Huduma za Mahakama. Hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa sheria mpya zilizotangazwa Agosti 27 ambapo sheria 49 zinapaswa kuanza kutumika kuanzia mwaka mpya.

No comments:

Post a Comment