Tuesday, August 31, 2010
Mh: Iddi Azzan, mgombea ubunge jimbo la kinondoni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi "CCM" amezindua kampeni zake rasmi katika viwanja vya Mwinjuma
Sandra Bullock Marks Katrina Anniversary at Clinic
Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu
Ummu Iyyaad
Tunaingia kumi la mwisho, kumi ambalo ndani yake kuna siku tukufu, siku ya Laylatul-Qadr, ambayo ibada yake ni bora kuliko ibada ya miezi elfu.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾ (( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ)) (( وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ)) (( لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ)) ((تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ)) (( سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ ))
KWA JINA LA ALLAAH MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU. ((Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr, (Usiku wa Makadirio[Majaaliwa]). Na nini kitachokujuulisha nini Laylatul Qadr?)) ((Laylatul-Qadr ni bora kuliko miezi elfu)) ((Huteremka Malaika na Roho (Jibriyl) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo)) ((Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri)) [Al-Qadr: 1-5)
Vile vile dalili katika Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu Fadhila za usiku huu mtukufu, na jinsi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa hali yake katika siku hizi kumi za mwisho za Ramadhaan.
Baada ya kuzijua fadhila zake usiku huu mtukufu inakupasa Muislamu ujikaze katika siku kumi hizi za mwisho kuacha mambo yote yanayokushughulisha ya dunia na utumbukie katika ibada tu ili uweze kuupata usiku huo mtukufu, yaani ukukute wewe ukiwa katika ibada ili zihesabiwe ibada zako
Tukifanya hesabu miezi elfu hiyo ni sawa na umri wa miaka 83!
1000 ÷ 12 = 83.3 yaani miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban.
Hivyo ikiwa Laylatul-Qadr imekukuta katika ibada ya aina yoyote, ikiwa ni Swalah (Qiyaamul-Layl), kusoma Qur-aan, kufanya aina za dhikr, kutoa sadaka, kulisha chakula, kuwasiliana na jamaa, kujielimisha au kuelimisha, kufanya wema kwa watu, yote hayo utaandikiwa kama umefanya hayo kwa umri wa miaka 83! Na juu ya hivyo ibada hiyo ya usiku mmoja tu ni bora zaidi kuliko ibada utakayoweza kufanya miaka 83 na miezi mitatu. Subhaana Allaah!
Jihadhari ndugu Muislamu usije ukakukuta usiku huu mtukufu ukiwa katika maasi au katika sehemu ukiwa umeghafilika na ya dunia kama sokoni, magenge ya soga au michezo ya kupoteza wakati au kwenye televisheni ukiangalia misalsalaat, mipira na sinema zikakupita kheri zote za usiku huu. Utaona siku hizi Waislamu wengi wanashughulika kwenda madukani kutafuta nguo za 'Iyd khaswa kina dada wakiacha masiku haya yawapite wakiwa humo badala ya kuwa majumbani mwao au misikitini kufanya ibada na kutegemea kuupata usiku huu.
Ni siku chache tu ndugu Waislamu ambazo zinakimbia kama upepo. Je, nani basi katika sisi atakayepuuza asiupate usiku huo? Na Nani katika sisi atafanya hima kuupata usiku huo? Kwani hatujui kama tutakuweko duniani mwakani kuzipata siku hizi au hata hatujui
Mwenye Kuukosa Usiku Huu Amekula Khasara Kubwa:
Hakika mwenye kuukosa usiku huo atakuwa amenyimwa kheri zake na itakuwa ni khasara kuukosa usiku huu mtukufu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : لَمَّا حَضَرَ رَمَضَان قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( قَدْ جَاءَكُمْ شَهْرُ رَمَضَان شَهْرٌ مُبَارَكٌ اِفْتَرَضَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ صِيَامَهُ تُفْتَح فِيهِ أَبْوَاب الْجَنَّة وَتُغْلَق فِيهِ أَبْوَابُ الْجَحِيم وَتُغَلُّ فِيهِ الشَّيَاطِين فِيهِ لَيْلَة خَيْرٌ مِنْ أَلْف شَهْر مَنْ حَرُمَ خَيْرهَا فَقَدْ حُرِمَ)) وَرَوَاهُ النَّسَائِيّ
Kutoka kwa Abu Huraryah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba ilipofika Ramadhaan, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi elfu. Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa haswa)) [An-Nasaaiy]
Siku hiyo ni siku iliyoteremeshwa Qur-aan kutoka mbingu ya saba hadi mbingu ya kwanza
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾ ((حم)) ((وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ)) (( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ)) ((فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ))
KWA JINA LA ALLAAH MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
((Haa Miym)) ((Naapa kwa Kitabu kinachobainisha)) ((Hakika Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji)) ((Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima)) [Ad-Dukhaan: 1-4]
Aya ya nne inayosema 'Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikma' kuwa kuna makadirio ya mwaka huo na yote yatakayotokea katika mwaka mzima. Kwa maana kwamba, siku ya Laylatul-Qadr, makadirio yote yaliyomo katika Al-Lawhum-Mahfuudhw (Ubao uliohifadhiwa) na huteremshwa haya makadirio na Malaika ambao wanaandika makadirio ya mwaka unaokuja yakiwa ni kuhusu umri wetu wa kuishi, rizki zetu, na yatakayotokea yote hadi mwisho wake. [Imesimuliwa na Ibn 'Umar, Mujaahid, Abu Maalik, Adh-Dhwahaak na wengineo katika Salaf – Ibn Kathiyr: 8:671]
Kujikaza kufanya ibada:
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa inapoingia kumi la mwisho akijikaza kwa kufanya ibada kuliko siku zozote zingine:
عن عائشة – رضي الله عنها- قالت: " كان رسول الله – صلى الله عليه وسلم- يجتهد في العشر الأواخر، ما لا يجتهد في غيره" مسلم
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika kumi la mwisho kuliko alivyojitahidi katika siku nyingine zozote" [Muslim]
Na katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim):
عن عائشة رضي الله عنها، قالت: "كان رسول الله صلى الله عليه وسلّم إذادخل العشر شذ مئزره، وأحيا ليله، وأيقظ أهله ( وفي رواية) "أحيا الليل،وأيقظ أهله، وجدّ، وشدّ المئزر" رواه البخاري ومسلم،.
Kutoka kwake pia Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha): "Ilipokuwa inaingia kumi (la mwisho) Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaza izaar (shuka) yake, akikesha usiku, na akiamsha ahli zake" (Na katika riwaaya nyingine) "Akikesha usiku, akiamsha ahli zake, akijitahidi na akikaza izaar yake" [Al-Bukhaariy na Muslim]
Kwa Nini Umeitwa Laylatul-Qadr?
Amesema Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Llaah):
Kwanza: Kutokana na uwezo nao ni utukufu
Pili: Ni usiku ambao una makadirio ya mwaka mzima na huandikwa yote yatakayotokea mwaka huo, na hii ni Hikma ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na kuonyesha usanifu wa utengenezaji Wake na Uumbaji Wake.
Tatu: Usiku huo una uwezo mkubwa
((من قام ليلة القدر إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه)) متفق عليه
((Atakayesimama usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia))[Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababu Ya Kupewa Waislamu Laylatul-Qadr:
Sababu ya kupewa Ummah huu wetu wa Kiislamu siku hii tukufu ya Laylatul-Qadr ni kwamba:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona umri wa Ummah za mwanzo ni mrefu, na umri wa Ummah wake ni mfupi akapewa usiku wa Laylatul-Qadr uwe ni bora kuliko miezi elfu. [Muwatwtwaa 1/321 (Muhammad Fuad 'Abdul-Baaqy]
Ibada Za Kufanya Masiku Kumi Haya Katika Kukesha:
1-Qiyaamul-Layl:(Kisimamo cha usiku kuswali)
((من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه)) متفق عليه
((Atakayesimama (Kuswali) Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
2-Kuosma Qur-aan:
Khaswa kwa vile usiku wa Laylatul-Qadr ndio usiku ulioteremeshwa Qur-aan
Vile vile Ramadhaan nzima inampasa Muislamu asome Qur-aan kwani ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 185]
Na Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alikuwa akimteremkia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kila usiku wa Ramadhaan akimsomesha na kumsikiliza Qur-aan:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ" رواه البخاري
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mbora (mwenye matendo mema) wa watu, na alikuwa mbora zaidi katika Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]
3- I'tikaaf:
Kutia nia kubakia msikitini kwa kufanya ibada tu humo kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo:
عن عائشة – رضي الله عنها- قالت "كان النبي يعتكف في كل رمضان عشرة أيام؛ فلما كان العام الذي قبض فيه اعتكف عشرين يوماً - أخرجه البخاري
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba: Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya I'tikaaf kila Ramadhaan siku kumi, ulipofika mwaka wake wa kuaga dunia alifanya I'tikaaf siku ishirini" [Al-Bukhaariy]
4-Kuomba Maghfirah:
Kwani usipoghufuriwa madhambi yako basi ni hatari!
عَنْ أَنَس وَغَيْره أَنَّ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا صَعِدَ الْمِنْبَر ثُمَّ قَالَ (( آمِينَ آمِينَ آمِينَ)) " قِيلَ يَا رَسُول اللَّه عَلَامَ مَا أَمَّنْت ؟
قَالَ (( أَتَانِي جِبْرِيل فَقَالَ يَا مُحَمَّد رَغِمَ أَنْف رَجُل ذُكِرْت عِنْده فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيْك قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل دَخَلَ عَلَيْهِ شَهْر رَمَضَان ثُمَّ خَرَجَ فَلَمْ يُغْفَر لَهُ قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل أَدْرَكَ وَالِدَيْهِ أَوْ أَحَدهمَا فَلَمْ يُدْخِلَاهُ الْجَنَّة قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ )) صحيح الترمذي و قال الشيخ الأباني حسن صحيح
Kutoka kwa Anas na wengineo kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipopanda juu ya minbar aliitikia ((Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn)). Alipoulizwa kwa nini ameitikia hivyo akasema: ((Amenijia Jibriyl akasema: Ewe Muhammad, ole wake yule ambaye unapotajwa hakuswalii, hivyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye umeingia mwezi wa Ramadhaan kisha akatoka bila ya kughufuriwa, kwa hiyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye amewakuta wazazi wake au mmoja wa wazazi wake lakini wasimuingize Peponi. Hivyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn)) [Swahiyh At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa Hadiyth hiyo ina daraja ya Hasan Swahiyh]
5-Du'aa Ya Kuomba Maghfirah Katika Siku Kumi Hizi Zakaatul-Fitwr Mwisho:
عن عائشة رضي الله عنها أنها قالت يا رسول الله أرأيت إن وافقت ليلة القدر ما أدعو قال: ((تقولين: اَللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌ تُحِبُّ الْعَفْو فَاعْفُ عَنِّي)) ابن ماجه و صححه الألباني
Kutoka kwa mama wa waumini bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba alisema "Ewe Mjumbe wa Allaah je, nitakapowafikiswha usiku wa Laylatul-Qadr niombe nini?" Akasema, ((Sema: Ewe Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe)) [Ibn Maajah na kaisahihisha Al-Albaaniy]
Matamshi Yake:
Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'Afwa Fa'afu 'Anniy
6-Kumkumbuka Allaah Kwa Aina Zozote Za Dhikr:
Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, Alhamdulillah, Laa Ilaaha Illa Allaah, Allaahu Akbar)
7- Kuomba Du'aa Na Haja Zako:
Kwa vile ni mwezi wa kuomba Du'aa pia kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala Ameunganisha Aayah za kufaridhishwa Swawm na Aaya za kuhusu kuomba Du'aa:
((وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُواْ لِي وَلْيُؤْمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ))
((Na waja Wangu watakapokuuliza khabari Zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka)) [al-Baqarah: 186]
Usiku Gani Khaswa Unapatikana Laylatul-Qadr?
Hadiyth zimetaja siku kadhaa ambazo usiku huu mtukufu hutokea katika siku kumi za mwisho na haswa katika usiku wa witiri, zikiwa zimetajwa nyingine kuwa ni usiku wa siku ya ishirini na moja, au ishirni na tatu, au ishirni na tano au ishirini na saba kama ilivyokuja katika dalili zifuatazo:
لحديث عائشة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((تحروا ليلة القدر في الوتر من العشر الأواخر)) رواه البخاري
Hadiyth kutoka Mama wa Waumini 'Aiashah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku za witiri kwenye siku kumi za mwisho)) [Al-Bukhaariy]
وفي حديث ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( التمسوها في العشر الأواخر من رمضان ليلة القدر في تاسعة تبقى ، في سابعة تبقى ، في خامسة تبقى)) رواه البخاري
Hadiyth kutoka Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan, katika (usiku wa) tisa, saba, na wa tano utakaobakia [mwisho wa Ramadhaan])) [al-Bukhaariy]
Imaam Ahmad amerikodi kutoka kwa 'Ubaydah bin As-Swaamit kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu usiku wa Laylatul-Qadr akasema:
((فِي رَمَضَان فَالْتَمِسُوهَا فِي الْعَشْر الْأَوَاخِر فَإِنَّهَا فِي وِتْر إِحْدَى وَعِشْرِينَ أَوْ ثَلَاث وَعِشْرِينَ أَوْ خَمْس وَعِشْرِينَ أَوْ سَبْع وَعِشْرِينَ أَوْ تِسْع وَعِشْرِينَ أَوْ فِي آخِر لَيْلَة ))
((Katika Ramadhaan, utafuteni siku kumi za mwisho, hakika umo katika siku za witiri, siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na tano, au ishirini na saba, au ishirini na tisa, au usiku wa mwisho)) [Ahmad]
Alama Zinazobainisha Laylatul-Qadr:
1. Kwenye usiku huo kunakuwa na mwanga zaidi.
2. Upepo siku hiyo hutulia, yaani siku hiyo hautokei upepo mkali.
3. Hali ya hewa huwa nzuri.
4. Nyoyo siku hizo huwa na utulivu na unyenyekevu zaidi kuliko siku nyingine.
5. Baadhi ya watu wema huoteshwa usiku
Asubuhi Yake:
حديث أبي بن كعب رضي الله عنه أنه قال : "أخبرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنها تطلع يومئذ ٍ لا شعاع لها" رواه مسلم
Hadiyth kutoka kwa Ubay bin Ka'ab (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Ametuambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa jua hutoka siku hiyo likiwa halina mishale (mikali)" [Muslim]
(( ليلة القدر ليلة طلقة لا حارة ولا باردة ، تُصبح الشمس يومها حمراء ضعيفة)) صحيح ابن خزيمة
((Laylatul-Qadr usiku ulio katika hali ya ukunjufu, usio na baridi wala joto, asubuhi yake jua huwa jekundu na dhaifu)) [Swahiyh Ibn Khuzaymah]
ليلة القدر ليلة بلجة (أي مضيئة) لا حارة ولا باردة ، لا يرمى فيها بنجم)) (أي لا ترسل فيها الشهب)
رواه الطبراني ومسند أحمد
((Laylatul-Qadr usiku wa kung'aa [yaani wenye mwanga] sio joto wala baridi, na vimondo (nyota za kufyatuliwa) hazitotumwa)) [At-Twabaraaniy na Ahmad]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kukesha masiku haya kumi ili tujaaliwe kuupata usiku huu mtukufu tutoke katika Ramadhaan hii tukiwa tumeghufuriwa madhambi yetu yote na tumepewa fadhila za usiku huu mtukufu zinazolingana na kuongezewa umri wa miaka 83. Aamiyn
Wassalaamu 'alaykum WarahmatuLlaahi Wabarakaatuh
MAREHEMU MUFTI MKUU, SH. HARITH BIN KHELEF AZIKWA
M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 42 (Sunday August 29, 2010)
It’s day 42 on M-Net’s Big Brother All Stars —and Sheila is evicted from the Big Brother All Stars house in show featuring Zambia’s Salma Dodia. She now joins Hannington, Lerato, Tatiana and Yacob in the Barn.
Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.
SIMBA KUPIMANA UBAVU NA MABINGWA WA KENYA J'MOSI
Ulinzi itaanza kucheza na Simba Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa,kabla ya kucheza Yanga Jumapili katika uwanja huo ambapo timu hizo zipo katika maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema leo kwamba timu inaendelea vizuri na mazoezi na kikosi cha timu hiyo kitaondoka kwa ndege septemba 12 kwenda Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi yao baada ya kuamua kutumia ueanja wa CCM Kirumba Mwanza.
HODGSON HAJISIKIA FURAHA

Siku moja baada ya kumtambulisha kwa mashabiki wa klabu ya Liverpool kiungo wa kimataifa toka nchini Ureno aliemsajili toka kwenye klabu ya FC Porto Raúl José Trindade Meireles, meneja wa majogoo wa jiji Roy Hogdson amesema anajisia furaha kumpata mchezaji huyo.
Roy Hogdson amesema kusajiliwa kwa kiungo huyo kwake ni kama amempata mkombozi katika safu ya kiungo ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikishindwa kuonyesha uhai toka alipoondoka Xavi Alonso na sasa ameondoka Javier Alejandro Mascherano.
Amesema mbali na kuondoka kwa wachezazni hao pia ifahamike juma lililopita alimuuza kwa mkopo kiungo wa kimataifa toka nchini Italia Alberto Aquillani katika klabu ya Juventus hivyo alikua na namna ya kumsajili mchezaji mwingine.
Mbali na Raúl José Trindade Meireles, kusajiliwa klabuni hapo, babu huyo wa kiingereza yupo katika taratibu za mwisho za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Fulham Paul Konchesky.
Paul Konchesky jana alikua uwanjani huko Anfield akiufuatilia mchezo wa ligi kuu kati ya Liverpool dhidi ya West Brom na inasemekana alikwenda jijini Liverpool kwa ajili ya kupimwa afya yake.
Mpaka sasa klabu ya Liverpool imeshafikisha idadi ya sita iliyowasajili katika kipindi hiki ambao ni Milan Jovanovic, Joe Cole, Christian Poulsen, Jonjo Shelvey pamoja na Danny Wilson.
MOHAMED KALLON AOMBA AWEKWE BENCH.

Mshambulaiji wa klabu ya Shaanxi Chanba ya nchini China Mohamed Kallon ameomba kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Sierra Leone kinachojiandaa na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012.
Mohamed Kallon amemuomba kocha wa timu ya taifa ya Sierra Leone Christian Cole kumuweka pembani katika mchezo huo dhidi ya Misri kwa sababu za kutokua Fit.
Mshambuliji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema maombi hayo kwa kocha Christian Cole, yamekuja kufuatia hatua ya kuuguza goti lake iliyochukua muda wa miezi miwili iliyopita.
Amesema kutokana na hatua hiyo hakupata muda wa kutosha kujiandaa akiwa na klabu yake ya Shaanxi Chanba, hivyo ameona ni bora aendelee kusubiri mpaka hapo atakapohisi yu fit kucheza soka kama ilivyokua zamani.
Kufuatia hali hiyo, Mohamed Kallon aliekua mchezaji bora mwenye umri mdogo katika fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 1996 ziliochezwa nchini Afrika Kusini amewataka mashabiki wa soka nchini Sierra Leone kutomfikiria vibaya kwa maamuzi aliyoyachukua.
TUPO TAYARI, TWENDE PAMOJA.

Huko nchini Afrika kusini, kikosi cha Bafana Bafana, nacho kinajiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Niger.
Kocha mkuu wa Bafana bafana Pitso Masimane amethibitisha kukiandaa vyema kikosi chake tayari kwa mchezo huo wa jumamosi ambao utapigwa nchini Afrika kusini.
Amesema mchezo wa kujipima ubavu dhidi ya Ghana ulimpa picha halisi ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza hivyo anaamini atalifanikisha suala la ushindi kwenye mchezo huo.
Nae nahodha wa kikosi cha Bafana Bafana Aron Makoena amesema wao kama wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao wanajua utakua mgumu kwa kila upande.
Makoena amesema wanatambua kilicho mbele yao ni kuhakikisha wanafuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zitakazochezwa nchini Equatorial Guinea pamoja na Gabon hivyo watacheza kwa kujituma zaidi.
Timu ya taifa ya Afrika Kusini imepangwa katika kundi la 7
Egypt , South Africa , Sierra Leone , Niger.
YES WE CAN!
YES we Can!hiyo ni kauli mbiu aliyokuwa akitumia rais wa Marekani Barrack Obama wakati wa kampeni za kuwania urais ambayo leo hii kocha wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mdenmark Jan Poulsen ameitoa akisema wanaweza kuifunga timu ya Algeria.
Stars inatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Algeria tayari kwa mechi yao ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa (CAN) itakayopigwa Septemba tano.
Akizungumza leo katika hafla ya kukiaga kikosi hicho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, Poulsen alisema kuwa pamoja na kucheza na timu iliyoshiriki kombe la dunia wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanashinda.
Awali Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera ambaye aliikabidhi bendera timu hiyo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kupamba na hatimaye kurejea na ushindi.
Aliwaasa wachezaji hao kujenga ari ya ushindi kinyume na hapo watakuwa wanashindwa kila siku na hiyo inatokana na sababu hawajaamua kushinda.
“Watanzania wamechoka, wanataka ushindi…ushindi hauletwi na TFF, wananchi au wadhamini ila ni ninyi, hivyo mhakikishe mnashinda mechi hiyo…haiwezekani tuwe wasindikizaji kila siku”, Alisema.
Bendera aliongeza kuwa licha ya wachezaji wa timu hiyo kubobea bado hawajawafurahisha watanzania, hivyo amewataka kutumia kila mbinu walizopewa na kocha wao kuhakikisha wanashinda.
Naye rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Leodger Chilla Tenga aliwataka wachezaji hao kutumia uzoefu waliona katika mashindano ya kimataifa ili kuweza kushinda na kuondoka na pointi tatu.
“Tunawafahamu Algeria katiKa soka kuwa ni wazuri, ni mechi ngumu na pia rahisi, ugumu wake ni kuwa wanacheza nyumbani, hivyo ninaamini mtaanza vizuri kwa kuondoka na pointi tatu”, Alisema.
Msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji 20 na viongozi watano utaondoka kesho mchana











