Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Thursday, September 30, 2010

CAR NEWS

26 hurt as 2 Metro buses collide in DC suburb

Two Washington Metro buses that collided are seen in Silver Spring, Md., Thursday, Sept. 30, 2010. Authorities say two Metro buses have collided in Silver Spring, injuring more than a dozen people. (AP Photo/Sarah Brumfield)
The Thursday morning accident comes a day after a tour bus carrying DC sightseers plunged off a highway in another Maryland suburb, killing the driver and injuring more than a dozen people.
Montgomery County fire department Assistant Chief Scott Graham says the 26 Metro bus injuries were not life threatening.
Eight high school students were involved. Montgomery County Public Schools spokeswoman Lesli Maxwell said the students suffered minor injuries and were taken to a hospital.
A spokesman for Montgomery County police said the accident was most likely weather related.

Matibabu ya bure CCRBT wenye fistula

Brenda Msangi kwa ushirikiano na Dina Marios alifika katika kituo cha redio CloudsFM kwa lengo la kuwahamasisha wakina mama wenye fistula kujitokeza popote walipo ili kutbiwa.

Fistula ni tatizo linalojitokeza kwa wakina mama wanaopatwa na tatizo wakati wa kujifungua ambapo kwa bahati mbaya njia ya kibofu cha mkono chaweza kupata tundu au njia ya haja ndogo kuchanika kiasi cha kuungana na njia ya haja kubwa na hivyo kusababisha mama kushindwa kuzuia haja ndogo, madhara ambayo husababisha kutokwa na haja ndogo mfululizo bila ya kuweza kuizuia.

Tatizo la fistula inatibika ikiwa mhusika atafika hospitali.

Kutokana na asili ya tatizo hili, akina mama wengi hupatwa na soni na kushindwa kutafuta matibabu, hivyo ninaungana na Brenda, Dina na wengine wote katika kuwahimiza ndugu, jamaa na rafiki kuwashauri na kuwasaidia akina mama wenye fistula kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu.

CCBRT inajitolea kugharimia usafiri, malazi, chakula na matibabu bure kabisa.

Ikiwa unalo tatizo, au unamfahamu yeyote mwenye tatizo hili, basi piga simu namba 0752 678263 POPOTE ULIPO na utaelekezwa jinsi ya kupata usafiri wa kufika hospitali ya CCBRT, Msasani, Dar es Salaam.

Hollywood Garter Girls


Beyonce doesn't mind breaking out the garters for a hot number, and she's not alone.

VODACOM MISS TANZANIA AAGWA NA KUKWEA PIPA KUELEKEA "MISS WORLD" NCHINI CHINA!


Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania akimuaga Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo wakati alipokuwa akiondoka kuelekea nchini China ambako atawakilisha nchi kwenye Shindano la Miss World 2010 litakalofanyika Oktoba 31 jijini Sanya.



Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akimuambia jambo kwa msisitizo Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel wakati alipokuwa akiondoka kweda Nchini China kwa ajili ya kushiriki shindano la Dunia Miss World 2010 kushoto ni Ibrahimu Kaude Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.



Bibi yake Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel Romana Mpangala akimuaga mjukuu wake kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere wakati alipokuwa akisubiri kupanda ndege kuelekea nchini China kwa ajili ya kushiriki shindano la Miss World 2010 litakalofanyika katika jiji la Sanya nchini humo, katikati ni9 mama yake Maria Mpangala.



Vodacom Miss Tanzania Genevive Emanuel akiwa katika picha ya pamoja na familia yake kutoka kulia ni Bibi yakeRomana Mpangala, Kaka yake Dunstan, Shangazi yake Julieth, mdogo wake Brian, na mama yake Maria Mpangala walipokwenda kumsindikiza wakati akielekea nchini Chini tayari kwa kambi ya Miss World 2010.



Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel katikati akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya Miss Tanzania na afisa kutoka Vodacom Tanzania kutoka kulia ni Aidan Rico, Bosco Majaliwa,Albert Makoye, Hashim Lundenga na Ibrahim Kaude Afisa Udhamini kutoka Vodacom Tanzania.

picha.  Full Shangwe 

16 SEMI FINALIST NAMED FOR THE EMERGING DESIGNERS COMPETITION!


Mama Shalua(Left),Charles Washoma(Middle) and Manju Msita on their judge duty.

Judges looking the sketch.


Sketches from different emerging designers who compete for Ermerging Designers Competition.

Three eminent Panelists Sit for Emerging Designer’s Competition Selection16 Semi Finalist Named for the emerging designers Competition.
“Contemporary Swahili” is the Theme of 2010 Competition
16 out of 31 neo talents have been selected as semi-finalist, for the Swahili Fashion Week 2010 Emerging Designer of the year Award.

The selection which was held on 29 September 2010 at the Southern Sun Hotel where 16 emerging designers were selected by a Panelist of Three Judges. The Judges were renowned designer Manju Msitta of Smart Afrika Design Label, Charles Washoma, CEO of African Life assurance and One of Dar es Salaams Fashionable man and Director of arts Nsao Shalua of Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council)

The selected 16 semi-finalist will once again yet undergo an Intensive Selection to select the 8 Finalist who shall compete for the prestigious title during the Swahili Fashion Week to be held in November this year.
Swahili Fashion week Fashion Coordinator Washington Benbella Commented “The response has been tremendous, and the Zeal and zest shown by the amazing talent we have in this country is phenomenal, but the journey of those who weren’t selected should not end here and not give up on their passion”

The semi-finals selections are Zarina Suleiman, Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urasa, ShaibMfaume, Annette Ngogi, Mwajabu Sadiki, Diana Malenge, Mgece Makory, Omary Bundalah, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Nadia. A. Ahmed, Angelina Muna, Jacqueline Chipeta, Bami Musese and Grace Kijo.
The judges were looking at various criteria to choose the candidates based upon the designers ability to sketch, sketch attractiveness, creativity, color and thematic relation.

Swahili Fashion Week is a platform for designers - both fashion and accessory – from Swahili speaking countries to showcase their creativity, market their art and network with their clientele. This is all aimed at promoting fashion as an income generating, job creating industry while emphasizing a “Made in East Africa “concept.
Initiating a dynamic and promising platform for the fashion industry in the region, Swahili Fashion Week is geared towards being the most sought out after fashion platform in Eastern Africa for the international market.
The third annual Swahili Fashion Week will take this November in Dar Es Salaam , Tanzania .

The competition, now in its third year has no age limit, and was open to anyone who believes he or she has the creative talent to be a fashion designer. “Swahili Fashion week is the perfect platform for a designer to showcases his creation, and the emerging designers competition, is a stage to jump start off ones career.” Added Mustafa Hassanali Swahili Fashion Week organizer.

KUFANYA KOSA SI KOSA - KOSA KURUDIA KOSA!

Wazanzibari wasikubali kurudi zama za ‘jino kwa jino’

Zipo dalili za wazi kwamba maadui wa demokrasia Zanzibar ambao hawakufurahia kuwapo kwa maridhiano kati ya vyama vya CCM na Cuf visiwani humo, wamedhamilia kuvuruga kampeni za uchaguzi zinazoendelea huko hivi sasa. Habari kwamba watu wasiojulikana wiki iliyopita na kwa nyakati tofauti, walipiga mawe misafara ya wagombea wawili wa kiti cha urais kwa tiketi ya vyama hivyo visiwani humo, zinatupa hofu kwamba safari ya Wazanzibari kuelekea kwenye maridhiano ya kudumu pengine itachukua muda mrefu sana.

Habari kutoka Zanzibar zinasema kwamba wakati msafara wa mgombea kupitia Cuf, Maalim Seif Hamad, ulipigwa mawe Ijumaa iliyopita katika Kijiji cha Bububu, msafara wa mgombea wa CCM, Dk Mohamed Shein, ulipigwa mawe sehemu hiyohiyo siku moja baadaye baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Misafara yote miwili ilishambuliwa saa 12 jioni ambapo baadhi ya wafuasi wa vyama hivyo walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Matukio hayo ya aibu yamekuja baada ya wiki kadhaa za kampeni safi na za kistaarabu miongoni mwa wagombea wa vyama vya Cuf na CCM ambao wamekuwa wakitoa matumaini kwamba uhasama kati ya vyama hivyo sasa umefika mwisho. Lakini katika hali ya kustaajabisha, kimetokea kikundi cha watu kinachodhihirisha waziwazi kubeba ajenda ya wahafidhina ambao tangu mwanzo hawakufurahishwa na mafanikio yaliyotokana na maridhiano yaliyofikiwa kati ya vyama hivyo vikuu visiwani humo.

Matokeo ya kura ya maoni ambapo asilimia zaidi ya 66 iliunga mkono kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, yalikuwa mwiba kwa baadhi ya Wazanzibari waliokuwa wananeemeka kutokana na hali ya kutofahamiana iliyokuwa imeshamiri kati ya wanachama wa vyama hivyo hasidi. Kwamba sasa vyama hivyo, viongozi na wanachama wake wanaelewana na kushirikiana katika shughuli zote za kijamii na maendeleo ni pigo kubwa kwa wahafidhina na wafuasi wao ambao sasa wanabuni mikakati ya kuirudisha Zanzibar katika zama za ‘jino kwa jino’.

Ndiyo maana tunalaani vurugu hizo kwa nguvu zote na kuvitaka vyombo husika kuchukua hatua haraka kabla vitendo hivyo havijatuzidi kimo, kwani ni dhahiri suala la viongozi wa Cuf na CCM kuwa kitu kimoja katika kutafuta mustakabali wa nchi yao ni dhoruba kubwa inayoyeyusha kabisa matumaini, matarajio na matamanio ya wahafidhina hao.

Ni ajabu iliyoje kwamba matunda ya maridhiano kati ya vyama hivyo yameanza kuonekana wakati huu wa kampeni ambapo wagombea wa vyama hivyo hawatoi tena lugha za matusi kwa wapinzani wao. Kinyume chake wanashindana na kupingana pasipo kupigana wala kukinzana, kwani sasa msingi mkubwa wa ushindani huu ni nguvu ya hoja, siyo hoja ya nguvu.

Juzi Maalim Seif Hamad aliwashangaza watu wengi waliohudhuria mkutano wake wa kampeni alipomsifia mpinzani wake, Dk Mohamed Shein, kwamba ni kiongozi bora ambaye anaweza kufanya naye kazi. Hayo ndiyo matunda ya maridhiano yaliyokomesha matusi, masimango na kejeli baina ya viongozi na wanachama wa vyama hivyo viwili na kuamsha hamasa na matumaini kwa Wazanzibari wa rika zote.

Kazi moja kubwa iliyobaki kwa Wazanzibari ni kushikamana na kushirikiana na vyombo vya dola katika kuanika wale wote wanaokwamisha juhudi za kuponesha vidonda vilivyotokana na kashikashi za kisiasa zilizodumu kwa miongo mitano hivi. Ni faraja na bahati iliyoje kwa viongozi kuonyesha njia kwa kutanguliza maslahi ya nchi badala ya binafsi, hivyo kuthibitisha pasipo shaka kwamba hakuna sababu ya wananchi kushindwa kwa kisingizio chochote kile.

Wakati zimebaki siku 33 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, ni imani yetu kwamba wananchi watahakikisha kwamba kampeni za uchaguzi zinazoendelea hivi sasa zinafanyika kwa amani na utulivu.
Habari kwahisani ya gazeti la Mwananchi.

CHADEMA NA VIONGOZI WA DINI WATETA


Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (katikati) akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati mgombea huyo alipokutana na viongozi mbalimbali wa dini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mgombea mwenza, Said Mzee Said.

Picture
Pichani ni Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati (kushoto), akizungumza na viongozi wa juu wa CHADEMA L-R = Freeman Mbowe, Willibroad Slaa na John Mnyika. (credit photo: Bashir Nkromo)

Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini inayosimamia masuala ya Rasilimali na Maadili, Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, na viongozi wengine wa dini waliokutana na CHADEMA wamekiasa chama hicho kufanya kampeni kwa misingi ya haki, utulivu na kukubali na kuheshimu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Viongozi hao wa dini walisema kuwa kukataa matokeo ni chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani na husababisha nchi kuingia kwenye matatizo makubwa kisiasa.

Wakawaomba viongozi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kushambuliana majukwaani, badala yake wanadi sera na Ilani za vyama vyao.

Dk. Slaa akizungumzia maombi ya viongozi hao wa dini kuwa wakubali matokeo yatakayotangazwa na Tume, alisema “tuliwaambia vurugu baada ya uchaguzi zinatokana na matokeo, nasi tumesema wao wasitwambie tu tupokee matokeo, ila wahakikishe taratibu za haki zinafuatwa katika kupata matokeo”.

Tume hiyo imekuwa ikuzungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu na tayari wameshakutana na Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na uongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Willibrod Slaa na John Mnyika.

SINGIDA LAZIMA TUSONGE MBELE…!!


Mgombea ubunge singida mjini Mohammed Dewji akionesha ishara ya vidole viwili kuwa ametumia bilioni 2.5 katika kuiletea singida maendeleo.

Na Hillary Shoo, Singida.

Mgombea ubunge wa jimbo la Singida mjini CCM,Mohammed Dewji, amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhaa tena wa kuwa mbunge wao ili aweze kuiendeleza singida na kuhakikisha inasonga mbele.
Dewji aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kindai mjini hapa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, akiwa kama mbunge ametumia zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kugharamia utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo aliahidi kwa kutumia fedha zake binafsi.
Dewji maarufu kwa jina la ‘Mo’ alisema endapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua tena kuwawakilisha bungeni, atahakikisha jimbo hilo linapaa zaidi kimaendeleo ili liweze kuwa mfano wa kuigwa nchini.
“Nasema tena kuwa dhamira yangu ni kuhakikisha kuwa singida tunasonga mbele kimaendeleo na kupaa zaidi kuliko kipindi kilichopita.”alisisitza MO huku akishangiliwa na wananchi.
Alisema kiasi hicho cha fedha, zimetumika katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005/2010 na pamoja ahadi zake binafsi.
Alisema utekelezaji huo ni pamoja na kugharamia miradi ya sekta ya afya ambapo amechangia zaidi ya shilingi 114.2.
“Katika sekata hii ya afya, nimetoa msaada wa vyandarua zaidi ya 22,000 kwa viijiji vyote vya jimboni kwetu, nimejenga wodi ya kulaza wagongwa wa macho, nimegharamia matibabu ya wagonjwa 520 wa macho, nimetuma msaada wa chakula kwa wagonjwa wa UKIMWI na nimewasaidia watu binafsi gharama za kuwapeleka kwenye hospitali za rufaa”alisema.
Katika sekta ya elimu, alisema amechangia zaidi ya shilingi 500 kugharamia miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata.
Dewji alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea urais, Jakaya Kikwete, amedai ameonyesha uwezo mkubwa katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.
Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Kindai Solomon Godfrey aliomba wananch kukichagua chama cha mapinduzi ili kuendeleza sera zake thabiti za kuongoza nchi kwa amani na utulivu.

MO akimnadi mgombea udiwani kata ya Kindai Godfrey Solomon.


Mgombea Ubunge Jimbo la Singida mjini MO akionekana akiimba pamoja na wananchi na wanachama wa CCM baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kata ya Kindai.

UN yatayarisha jopo la uchunguzi DRC

Umoja wa Mataifa unasema unatayarisha jopo la maafisa wa ngazi za juu kusikiliza ushahidi kutoka kwa waathirika wa ubakaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, ambako maelfu wanabakwa kila mwaka.
Umoja wa Mataifa watayarisha jopo la uchunguzi kwa waathirika wa ubakaji DRC.
Picha VOA TV
Umoja wa Mataifa watayarisha jopo la uchunguzi kwa waathirika wa ubakaji DRC.

Umoja wa Mataifa unasema unatayarisha jopo la maafisa wa ngazi za juu kusikiliza ushahidi kutoka kwa waathirika wa ubakaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, ambako maelfu wanabakwa kila mwaka.
Jopo hilo litaanza kukutana Alhamisi Septemba 30 katika mji wa Bukavu, mashariki mwa Congo na litasikiliza ushahidi kutoka kwa watu waliobakwa katika majimbo kadhaa hadi Oktoba 10. Soma zaidi: voanews

IDADI YA WAKIMBIZI IMEPUNGUA - PINDA (UN. NDANI YA NEW YORK CITY)

Picture
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) wakiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Ban Ki Moon (watatu kulia ) na Nibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Dr. Asha Rose Migiro (wanne kulia) kwenye Ofisi za Umoja huo Mjini New York Septemba 27, 2010.
Idadi ya wakimbizi nchini imepungua kutoka milioni 1.2 mwaka 1994 hadi  100,000 waliopo hivi sasa. Kutokana na hilo, kambi 12 zimefungwa, jambo linalodhihirisha utulivu umerejea kwenye nchi zao.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema hayo juzi, alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa niaba  ya Rais Jakaya Kikwete. Alisema Tanzania pia imetoa uraia kwa wakimbizi 162,254 walioingia nchini tangu mwaka 1972. Wamepatiwa uraia chini ya utaratibu ulioanzishwa baada ya uhuru. “Idadi ya wakimbizi imepungua kutoka milioni 1.2 mwaka 1994 hadi 108,426 ilipofika Julai 31, mwaka  huu. Serikali hivi sasa inajaribu kuwashirikisha waliopewa uraia katika jamii ya Watanzania,”  alisema.

Hata hivyo, alisema kazi ya kuwajumuisha katika jamii ya Watanzania wakimbizi hao waliopewa uraia ina  gharama kubwa, ambapo dola za Marekani milioni 146 (sh. bilioni 200) hutumika.

“Huo ni mzigo mkubwa kwa nchi masikini kama Tanzania. Tunaiomba jumuia ya kimataifa kuunga mkono  mradi huu, chini ya kanuni ya kuwajibika kwa usawa na kubeba mzigo kwa pamoja,” alisema.

Wakimbizi wanaopewa uraia ni waliokaa muda mrefu au kuzaliwa nchini, ambao hawajui waende wapi na wanaridhishwa na maisha ya Tanzania, hivyo kuomba kisheria kuwa raia kwa ridhaa yao. Waziri Mkuu Pinda alisema Tanzania itaendelea na jitihada za kudumisha amani, kuleta haki na  maendeleo katika Bara la Afrika na kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kufanikisha azma hiyo.

Alisema Tanzania itajitahidi kutekeleza wajibu wake katika kutimiza malengo manane ya Maendeleo ya Milenia na kuitaka jumuia ya kimataifa kuwa na mshikamano, ili kufanikisha malengo hayo. Waziri Mkuu awali alikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, aliyeisifu  Tanzania kwa kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia. Kwa upande wake, Pinda alimshukuru Ban kwa kumteua Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kusimamia mchakato wa  kura ya maoni Sudan na Dk. Augustine Mahiga kuwa mjumbe wa Katibu Mkuu katika kufuatilia amani ya Somalia.

CHADEMA WAWATIMUA UV-CCM KATIKA SHULE YA UMMA

Mtoto wa mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwani Kikwete leo ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.

Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu, walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.

Kabla ya msafara wa Ridhiwani kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho, aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo, Msambatavangu, alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Raisi Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.

Hata baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo, bado msafara huo ulifika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.
Credit: Francis Godwin
Picture
Darasa la S/Msing Ipogolo lililokuwa limeandaliwa kwa ajiliya kikao cha UV-CCM
YOTOKANAYO...

Vyombo mbalimbali vya habari vimesharipoti na kulaani mkanganyo unaofanywa katika kampeni za Kisiasa, ambapo chama kilichoko madarakani kinatumia mwanya huo kushindwa kutofautisha shughuli za Kisiasa za Chama na shughuli za Kiserikali. Magazeti yamesharipoti kuhusu Wafungwa kutumiwa katika ujenzi wa majukwaa ya kisiasa na hivi jana imeripotiwa habari ya Wanyamapori kuwindwa ili kuwapatia kitoweo walioongozana katika shughuli za Kisiasa za Chama, na katika wananchi wakauziwa kitoweo (kuzuga?).

Wanaofanya hivi wanafanya kusudi ili kuonesha kuwa wao ni "mwamba" na hakuna wa kuwafanya lolote?
Wanafanya dharau, au ni kwamba hawafahamu kuwa wanalofanya ni kosa?

Kama si dharau  ya umuhimu wa elimu, ni kwa nini mikutano ya kisiasa iendeshwe mashuleni? Juzi tu hapa tumeshangazwa na kitendo cha wanafunzi kutokuingia madarasani, ati wanasubiri msafara wa mgombea uraisi upite? Ama, kwa utaratibu upi jama? Mbona hatuna heshima kwa mambo ya msingi kama elimu?

Mimi kinachonifurahisha ni kwamba, wananchi wameshaona huu sasa ushakuwa ujinga. Hizi ndizo chokochoko zinazoamsha hasira na kusababisha watu watwangane makonde... na zaidi ya hapo. Haya!

VODACOM MISS TANZANIA 2010 AKABIDHIWA BENDERA, KWENDA CHINA KESHO

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA SEKTA BINAFSI TANZANIA ESTHER MKWIZU AKIMKABIDHI BENDERA YA TAIFA VODACOM MISS TANZANIA 2010, GENEVIEV EMMANUEL MPANGALA.


GENEVIEV AKIWA NA MISS TANZANIA ALIYEMALIZA MUDA WAKE, MIRIAM GERALD.


WAZAZI WA MISS TANZANIA.

Wednesday, September 29, 2010

Back Home

Knight And Day" Tokyo Premiere

Actor Tom Cruise (L) and actress Cameron Diaz pose during the Japan Premiere of 'Knight and Day' at Roppongi Hills on September 28, 2010 in Tokyo, Japan. The film will open on October 9 in. 

Dancing With The Stars: Week Two Results And Elimination

dancing-with-the-stars-week-two-elimination-results-derek-hough-jennifer-grey
On last night’s episode of ABC’s Dancing With The Stars we watched as the couples performed the Jive and the Quickstep, with some stars getting better while others showed no improvement at all. Tonight, one couple will be eliminated, and if you think you know who goes home, you may want to rethink that! Keep reading for all the details and find out who got eliminated this week!

dancing-with-the-stars-kurt-warner-dishes-about-show
ABC’s Dancing With The Stars celebrity dancer, Kurt Warner has had two great performances so far on the show. Kurt recently chatted with ESPN about his experience and his dance partner, Anna Trebunskaya. Keep reading for more details and to hear why Kurt is doing the competition!

Mariah Carey falls on stage during performance in Singapore – Video



The pop diva, Mariah Carey fell on stage while she was performing at a concert in Singapore on Saturday, September 25, 2010.The singing sensation was entertaining a huge crowd by performing her 1992 hit single "Make It Happen" at the Singapore Grand Prix over the weekend when she tumbled on stage.Although, 
Mariah Carey fell on stage in front of a huge audience, it didn't affect the energy and magic of her performance.After her fall, backup dancers helped Mariah Carey and the pop legend singer continued with her flawless performance and made fun of herself by saying that she meant to do that.Shortly after Mariah Carey had fallen on stage, an assistant rushed alongside her and eventually took away from Mariah the high heels that were possibly the cause of the embarrassing fall.The 40-year-old singer, Mariah Carey also tweeted regarding that falling incident.The same incident had happened to Alicia Keys in July, while she was four months pregnant and performing during a show at the Essence Music Festival in New Orleans.

BIG BROTHER ALL STARS







Meryl is evicted from the Big Brother All Stars house in show featuring performances from former Housemates. She now joins Lerato, Tatiana, Sheila, Paloma, Jen and Code in the Barn. It’s day 70 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Meryl is evicted from the Big Brother All Stars house in show featuring performances from former Housemates. She now joins Lerato, Tatiana, Sheila, Paloma, Jen and Code in the Barn. Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Picture By Multichoice Tanzania .

ROONEY NJE WIKI TATU !!!!!!!!


Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Man Utd kitakachocheza hii leo mchezo wa pili wa makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Valencia huko nchini Hispania, mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney imefahamika atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma matatu yajayo.

Taarifa zilizotolewa na meneja wa klabu ya Man utd Alex Ferguson alipozungumza na waanduishi wa habari hapo jana zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa kipindi cha majuma matatu kufuatia majibu ya vipimo alivyofanyiwa mara baada ya kuumia kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma lililiopita dhidi ya Bolton Wanderers.

Alex Ferguson amesema licha ya kutegemea mshambuliji huyo kuwa nje kwa kipindi cha majuma matatu, bado inawezekana kurejea uwanjani baada ya majuma mawili nah ii inategemea na huduma ya matibabu anayoendelea kup[atiwa kwa sasa huko jijini Manchester.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 68 pia amemzungumzia kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Paul Scholes ambae nae anasumbuliwa na maumivu ya kiazi cha mguu ambayo huenda yakamuweka nje kwa kipindi cha siku kumi.

Diego López Rodríguez KUSAJILIWA EMIRATES.


Meneja wa klabu ya arsenal Arsene Wenger amelazimika kurejea tena sokoni kusaka kipa mbadala wa Manuel Almunia ambae ameendelea kuwadhihirishia wengi kwamba hastahili kuwa chaguo lwa kwanza la mzee huyo wa kifaransa msimu huu.

Arsene Wenger ameingia sokoni kwa mara nyingine tena huku jicho lake akilitupia huko nchini Hispania kwenye uwanja wa El-Madriga yalipo makao makuu ya klabu ya Villareal kwa kutaka kumsajili kipa wa kimataifa toka nchini Hispania Diego López Rodríguez.

Taarifa toka nchini Uingereza zimeeleza kuwa tayari utaratibu wa uhamisho wa kipa huyo umeshaanza kuchukua mkondo wake na kuna uwezekano mkubwa wa kuelekea Emirates kitakapofika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi januari mwaka 2011.

Lopez, mwenye umri wa miaka 28, pia na sifa ya kucheza beki wa pembeni hatua mbayo imeelezewa kuwa faida kwa klabu ya Arsenal endapo watamsajili na watapenda kumtumia katika nafasi hiyo kwenye baadhi ya michezo inayowakabili msimu huu.

BALITELLI KUREJEA DISEMBA


Uongozi wa klabu ya Man city umetoa taarifa za amendeleo ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini italia Mario Balotelli alien nje ya uwanja kwa sasa akiuguza jeraha la goti alilolipata siku chache baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Inter Milan ya nchini italia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mario Balotelli ataendelea kuw anje ywa uanjwa na huenda akaonekana tena uwanjani baada ya majuma sita ama manane baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Uongozi wa klabu ya Man City umeeleza kwamba mshambuliaji huyoa naendelea vyema na wanamatumaini kwa kipindi alichopangiwa cha majuma sita ama manane atarejea katika hali ya kawaida na kuitumikia klabu hiyo ipasavyo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alitegemewa huenda angerejea uwanjani kati kati ya mwezi ujao, lakini imeonekana bado atahitaji kipindi kingine cha kuendelea kuuguza jeraha lake kufuatia upasuaji aliofanyiwa.

Akizungumza na vyombo vya habari hii leo wakati akirejea nyumbani kwao mjini Milan nchini Italia Balotelli amesema anasikitishwa na taarifa hizo lakini hana budi kusubiri kama ushauri wa daktari unavyoeleza.

Muda wa kurejea uwanjani kwa mshambulaji huyo huenda ukawa ni muda muafaka kufuatia kalenda kuonyesha kuwa mnamo Desemba 16 mwaka huu klabu yake ya Inter Milan itakua na mchezo wa ligi ya ulaya dhidi ya klabu ya Juventus ambayo itakua nyumbani mjini Turin.

SOKA MAREKANI KUITANGAZA TANZANIA


Pichani ni Rais wa Soccer , Patrick Steenberge.

Chuo Kikuu cha Drake cha Marekani na Chuo cha CONADEIP cha Mexico wanatarajiwa kutangaza mpira wa Marekani Mei mwakani utakaofahamika kama Kilimanjaro Bowl, kwa sababu Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye maeneo ya kihistoria na utalii. Rais wa Global Soccer, Patrick Steenberge, amesema leo kuwa Mei 17, 2011 kutakuwa na matukio mawili likiwemo la kliniki ya mchezo huo itakayofanyika mkoani Kilimanjaro na kuzuru zaidi ya robo ya vivutio vya kitalii ikiwamo Mlima Kilimanjaro.Steenberge alisema Mei 21 timu za vyuo hivyo zitamenyana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCOB’s), kabla ya kutembelea vituo vya yatima.Naye Kaimu Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi, alisema ujio wa timu hizo utaitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya michezo na utalii.

USADF EXTENDS FUNDING TO MARGINALIZED TANZANIANS

In an effort to support grassroots groups in Tanzania, the United States African Development Foundation has signed three grants which will benefit HomeVeg Tanzania Limited (HomeVeg) and Manyara Ranch Livestock Producers.
Association (MRALIPA).
Picture

After signing the grant, USADF President Lloyd Pierson stated, “USADF’s mission is working with the most marginalized populations. These new grants provide support for some of the most underserved groups in Tanzania to support their ideas for income generating projects.”

Located in Arumeru District, Arusha Region, HomeVeg works with small-scale vegetable growers to increase their profitability by linking them to reliable markets in Europe. HomeVeg organizes famers and pays them a fair wage for the produce that they provide. After collecting the produce from the farmers, HomeVeg places the vegetables in a cold chain system in order to maintain the specific temperature that will preserve the vegetables and ensure compliance with consumer demands market requirements in its European markets.

HomeVeg is looking to work with smallholder farmers in Meru, where the collapse of the coffee industry there impoverished many of these farmers.  Farmers there need an alternative high-value export crop to ensure that they can make an adequate living on their small plots of land. The grant will provide funds for training, development of a business plan, obtain global certification, and procure equipment needed process and store vegetables.

MRALIPA is a registered Livestock Producers Association works to improve the quality of livestock raised and capture a greater portion of the local market for meat.   The group was formed by small scale farmers hailing from seven separate villages surrounding the Manyara Ranch in Monduli District of the Arusha Region.
MRALIPA fits squarely within ADF’s focus on serving marginalized populations.  The Association is made up of Maasai pastoralists, which is a group that has been traditionally disadvantaged and have largely operated outside the formal sector economy..  USADF funding will finance training in marketing and business development, training in livestock, access to microloans for farmers, and link farmers to market opportunities.

USADF began programming in Tanzania in 1986.   Tanzania’s current portfolio stands at twenty-nine investment projects totaling $5.4 million.

WAPINZANI UMOJA TRANS

Vyama 14 vya kisiasa vya ushindani mkoani Iringa vimeungana na kumsimamisha mgombea mmoja, Mariam Mwakingwe wa NCCR-Mageuzi ili kuwania Ubunge kwa jimbo la Iringa Mjini ili  kuongeza nguvu ya upinzani dhidi ya Monica Mbega wa CCM na Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA.


Vyama vinavyounda umoja huo ni NCCR- MAGEUZI , TLP, TADEA, SAU, CHAUSTA, APPT-MAENDELEO, JAHAZI-ASILIA , CUF, NLD, UDP, MAKINI, DP, AFP NA UPDP.
Picture
Gari hili lililosheheni bendera ya Taifa na nyingine za vyama vya Kisiasa nchini Tanznaia, ni moja ya magari yanayotumiwa na muungano wa vyama vya upinzani (isipokuwa CHADEMA) kwa shughuli za kampeni Iringa). Umoja huo umemsimamisha mgombea mmoja wa ubunge kwa jimbo Iringa Mjini, Mariam Mwakingwe wa NCCR- Mageuzi (credit photo: Frank Leonard/HabariLeo)

WAZIRI MKUU PINDA AHUTUBIA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA..!!!


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York alikomwakilisha Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Aiowa nchini Marekani wakti alipotembelea Chuo hicho Septemba 25, 2010.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010. Katikati ni mkewe Tunu.

NITAWASHTAKI MSIPOKUWA MAKINI – WAZIRI MAGUFULI…!!!


Magufuli ambaye ni Waziri wa uvuvi na maendeleo ya mifugo alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua jengo hilo jipya lenye umbo la samaki ambalo linatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh3.5 bilion likiwa na vyumba 80 vya ofisi pamoja na sehemu ya kuegesha magari zaidi ya 50.Jengo hilo linalo jengwa na mkandarasi toka china pamoja na mshauri mwelekezi kutoka Archquants Services Ltd

Ukwamishwaji wa kazi ya ujenzi huo kwa sababu ya mvua zilizotolewa na mshauri huyo pamoja na mkandarasi wake zimelenga kutaka walipwe zaidi na kwamba serikali haipo tayari kukubaliana na utetezi huo kwa kuwa si sababu za msingi.alisema waziri huyo

‘‘Hizo sababu zenu si za msingi, hivyo sizikubali kwa kuwa mvua haizuii kukamilisha ujenzi. Hivyo nataka ujenzi huo ukamilike Novemba 30 kama ulivyopangwa na si Desemba kama mnavyotaka ninyi… kama mlitegemea kulipwa fedha zaidi, hamtalipwa wala hamtaongezewa muda wowote wa ziada,’’

Aliongeza kusema: “Endapo mtashindwa kukamilisha ujenzi huo kama mlivyowekeana mikataba, tutamchukulia hatua za sheria makandarasi ili tuwakate fidia kutokana na kushindwa kuheshimu mkataba,’ aliongeza Awali mshauri mwelekezi wa jengo hilo, Barongo Charles Mutalina aliomba kuongezewa muda wa kukamilisha ujenzi huo hadi mwishoni mwa Desemba kutokana na kuwepo na mvua kwa misimu kadhaa tangu ujenzi huo ulipoanza mwezi Machi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa -MTWARA


Ziara ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Mkoani Mtwara ambapo amekutana na wanachama wa UWT katika mikutano ya ndani na kuwahamasisha umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani Oktoba 31, mwaka huu na kupiga kura hapa akiwahutubia wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano wake. Picha zote na Mwanakombo Jumaa.


Hawa ni baadmbehi yawagoa Udiwani wa Jimbo la Masasi (MTWARA) wakinadiwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa CCM tawi la Mwenge B-Tandahimba