Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Tuesday, November 30, 2010

Haya Ndio Maonyesho ya Mitindo ya Victoria’s Secret Ndani ya NYC


Mambo ya show ya Victoria’s Secret. mdada Mwana mitindo Maryna Linchuk pole pole mwendo wamaringo na zake pozi, akikatiza kwenye njia ya kujidai katika show ya Victoria’s Secret 2010 jijini New york City.

Hii ndio hali halisi show ya Victoria’s Secret kama tunavyomuona mwanamitindo Candice Swanepoel anavyojivinjari ndani ya 18 kama yuko down town kwenye show ya mitindo ya Victoria’s Secret iliyo fanyika Nov 10,2010 Jijini NEW YORK CITY.


Mwana mitindo Lily Donaldson akijimwaga kwa mapigo ya chapa nikuchape, nyuma kimtindo wa tausi denge wafahari, huku akijipinda kama al batwaah anaevutiaa, kwenye show ya Victoria’s Secret  iliyofanyika kwenye mitaa ya Lexington Avenue Armory November 10, 2010 Jijini New York City. (Picha kutoka kwa albamu ya Theo Wargo)

KIZAZA CHA KOMBE LA CHALENJI: MALAWI YATOKA MIKONO JUU KWA USHINDI WA 3-2


MSHAMBULIAJI wa harambee stars akishambulia langoni mwa Malawi, timu hizo zilipomenyana leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo kwenye mtanange wa michuano la Kombe la Chalenji. Shambulio halikuzaa matunda kutokana na kuokolewa na mabeki ya Malawi. Hatimaye Harambee ilitoka uwanjani ikiwa imejiinamia kwa kutwangwa mabao 3-2

Barcelona Yatoka Mikono Juu Baada Ya kuibamiza Real Madrid C.F Bao 5-0 Bila ya Huruma!


Jose Mourinho amekataa kukubali yakuwa jana timu yake imeaibishwa baada ya kukubali kichapo cha mabao 5 kwa 0 toka kwa wapinzani wao wakubwa timu ya Barcelona. Magoli yaliofungwa na Xavi, Pedro, na mawili ya David Villa na msumari wa mwisho kupigiliwa na Jeffren, yliifanya timu ya Real kupoteza mwelekeo kabisaa na kumfanya kocha huyo aingie doa baada ya kupata kipigo cha kwanza toka ajiunge na klabu hiyo inayotumia dimba la Santiago Bernabeu.

Mara nyingi mechi kubwa kama hizi hazikosagi vituko na kituko cha kwanza kilitokea baada ya Cristiano Ronaldo kumsukuma kocha wa Barcelona Pep Gardiola wakatik kocha huyu alipokataa kumpa mpira Ronaldo, nae beki Sargio Ramos alizawadiwa kadi nyekundu nakuicha Real wakiwa pungufu ya mtu mmoja.

Mourinho alidai kuwa “hakuna timu ilioaibishwa bali timu moja imeshinda na nyingine imeshindwa, hatukucheza vizuri kabisa na wao walicheza vizuri na tuliwazawadia magoli mawili baada ya uzembe wiki iliyopita tulikuwa juu nawao leo wapo juu”

“NASEMA NATAKA KUWA MSAADA KWA TIMU YA ENGLAND” – ANDREW CARROLL…!!!

Mshambuliaji anae chipukia kwa kasi wa Newcastle utd Andrew Carroll amesema anataka kuweka pembeni majanga yaliomkuta ambayo yamemfanya awe anaonekana mahakamani mara kwa mara na kuwa mcheza muhimu kwa Taifa lake.

Kinda huyo ambae mpaka sasa amekuwa ni miongoni mwa wafungaji wanaongoza kwa magoli katika ligi kuu nchini Uingereza anataka kufata nyazo za akina Alan Shearer nakuwa karibu na Wayne Rooney katika timu yao ya taifa ambayo mara ya mwisho ilikubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Ufaransa katika mechi ya kirafiki.

Katuni yetu ya leo!

PEACOCK HOTEL KUADHIMISHA MIAKA KUMI YA USIKU WA MTANZANIA

Kiongozi wa bendi ya Sikinde, habibu Mgalus akizungumza na waandishi wa habari jinsi bendi hiyo itakavyoshiriki Tamasha hilo. Kushoto ni mwanamuziki wa bendfi hiyo, Rehani Bitchuka na wengine kutoka kulia ni Wakurugenzi wa Hoteli ya Peacock, Joseph Mfugale na Damasi Mfugale.

Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania. Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. 

Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu. Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku. Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star. Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. 

Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi. Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Damas Mfugale kwa namba 0789-280112

NMB BANKI YAIONGEZEA NGUVU KAMPENI YA TANZANIA 50 PLUS….!!!


Msemaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Shy-rose Bhanji (kushoto) akimkabidhi vipeperushi vitakavyotumika katika utoaji elimu juu ta saratani ya tezi dume kwa Mwanzilishi wa Kampeni hiyo Dr. Emmanuel J. Kandusi (kulia) huku Balozi mstaafu George Maige Nhigula ambaye ni mshauri katika bodi ya Taasisi hiyo akishuhudia makabidhiano hayo.

Benki hiyo imechangia vipeperushi vipatavyo 35,000 ambavyo vitatumika kufikisha ujumbe na kutoa Elimu zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Saratani ya tezi dume. Rais wa PHEN Bw. Thomas A. Farington alisema kuwa wanaishukuru sana benki hiyo kwa msaada huo na uwe ndio mwanzo wa misaada mingine zaidi katika kuongeza jitihada za kupambana na gonjwa hili linaloendelea kukua kwa kasi katika nchi nyingi za Kiafrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Lengo kuu la vipeperushi hivi litakuwa ni kuwaelezea Watanzania ni nini chanzo, dalili na umuhimu wa kufanya vipimo dhidi ya gonjwa hili. Zifuatazo ni picha za matukio wakati wa makabidhiano ya vipeperushi hivyo.


Mkurugenzi Mkuu wa MAN MAGAZINE Bw. Dismas Massawe (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya jarida lake ambalo linahusiana na wanaume litakavyosaidia usambazaji wa vipeperushi hivi. Kila nakala ya Jarida hili ndani yake kutakuwa na kipeperushi hicho.(kushoto) Mwanzilishi wa Kampeni za Tanzania 50 Plus Dr. Emmanuel J. Kandusi

LEO RAIS KIKWETE AKUTANA NA BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI

RAIS Jakaya Kikwete akizungumza na mawaziri wake, leo Ikulku mjini Dar es Salaam.

Mawaziri wote wakiwa katika kikao hicho na rais Kikwete leo (Picha zote na Freddy Maro)

MH MIZENGO PINDA AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOREA YA KUSINI…!!!


Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Korea Kusini, Bw.Kim Jae-Shin aliyeameambatana na Balozi wa Korea ya Kusini nchini Tanzania , Bw Young Hoon Kim(hayupo pichani) Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda(katikati) akizungumza Balozi wa Korea ya Kusini Nchini, Bw Young Hoon Kim(kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea ya Kusini, Bw Kim Jae-Shin(kushoto) katika viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu mara tu baada ya Mazungumzo yao jijini Dar es Salaam Novemba 30th,2010 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

REMIX KENYAN NA WATANZANIA UHURU NA UMOJA MAKAMUZI PARTY NDANI YA WASHINGTON DC!


Monday, November 29, 2010

Barty Cake Sasa Yuko Kamili Kamili Kukupikia Cake na Vyakula!

Kwa wale wenye shuhuli za kijamii zinazojitokeza kila wikiend. Bibie Bartlet Kamna. Anapikisha vyakula, pamona na kutengeneza Cake za Birthaday Harusi N.K. Sasa amejitambulisha na kujitokeza rasmii. Bartlet Kamna ni mtanzania halisi mkazi wa Riverdale, Maryland. Kwa tarifa zaidi usikose kumtembelea kwenye blog yake. Click Barty Cake Test Of Tanzania.  

Marijani Raajab - Mwanameka!

WAKIFUNGWA MOJA LAZIMA YAPILI WAPOTEZE USHINDI!



Ama kweli sikio la kufa halisiki dawa!, mechi nyingi wanazocheza Washington Redskins, huwa nikama kawaida yao, wakishinda moja mechi inayofuata lazima wafungwe. Hii inawaumiza sana wapenzi wa timu hiyo. Katika michezo ya NFL American Football inayoendelea kila mwisho wa wiki jijini hapa.

Mchezaji wa Washington Redskins Santana Moss aliokua chini akificha mpira, huku kizaza cha wachezaji Minnesota Vikings linebacker E.J. Henderson (56), cornerback Antoine Winfield (26) na defensive tackle Pat Williams (94) wakimvamia kutaka kupora mpira aliuficha mapajani, kwenye kipindi chapili cha mchezo wa NFL football uliochezwa jana jumapili Nov.28/2010 kwenye uwanja wa Washington Redskins Landover, Md. Picha kwahisani ya (AP/Pablo Martinez Monsivais)

Zanzibar Heroes Yatoka mikono juu. Baada ya kuifunga Sudan 2-0!


Ali Ahmed Salum Shibiri akishangilia baada ya kuipachikia bao la pili na la ushindi, timu yake ya Zanzibar Heroes, timu hiyo ilipomenyana na Timu ya Taifa ya Sudan,  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu ya Manchester united Wachukua Golikipa mpya!

 
Hatimae klabu ya Man Utd imekamilisha taratibu za usajili wa kipa wa kimataifa toka nchini Denmark na klabu ya Aalesund Anders Lindegaard. Man utd wamekamilisha dili la kumsajili kipa huyo huku malengo yao makubwa yakiwa ni kutaka kumrithisha nafasi ya kipa wa sasa Edwin van der Sar ambae tayari ameshatangaza kutundika gloves mwishoni mwa msimu huu. 

Man Utd wamekamilisha dili hilo baada ya mazungumzo kati yao na uongozi wa klabu ya Aalesund ya nchini Denmark kukamilika siku mbili zilizopita ambapo mashetani wekundu walitakiwa kutoa kiasi cha paund million 3.5 kama ada ya uhamisho ambayo tayari imeshalipwa. Hata hivyo kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 atajiunga na klabu ya Man Utd kitakapofika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka 2011.  

Meneja wa klabu Man Urd Sir Alex Ferguson amemwagia sifa kedekede kipa huyo huku akisema ana uwezo mkubwa ambapo anaamini utawasaidia katika harakati za kuziba nafasi ya Edwin van der Sar. Wakati Ferguson akimsifia kipa huyo kipa wa zamani wa klabu ya Man utd Peter Schumacher ameuponda usajili huo huku akisema Anders Lindegaard hana uwezo wa kutosha wa kuitumikia klabu hiyo ipasavyo.

Tottenham Tatoka Mikono Juu Dhadi Ya Liverpool!






Timu ya liverpool yabamizwa bao 2-1 na Tottenham.

WAZIRI HAWA GHASIA APONGEZWA NA WAFANYAKAZI WA UMMA!


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. George Yambesi (kulia) na Mkutugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) mara baada kuwasili kuanza majukumu yake leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia (kulia) akikaribishwa kwa furaha na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili Ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili Ofisini kwake mapema asubuhi ya leo. Pamoja na mambo mengine amewataka wafanye kazi kwa bidii ili kuimarisha Utendaji katika Sekta ya Umma nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Umma Bi. Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini leo (Picha na Aron Msigwa- MAELEZO)

Mh. John Zefania Chiligati Akimkabidhi Nyaraka Mh. Prof. Anna Tibaijuka!

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. John Zefania Chiligati (kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali za kutendea kazi Waziri mwenye dhamana hiyo Mh. Prof. Anna Tibaijuka. Makabidhiano hayo yalifanyika mara baada ya Mh. Tibaijuka kuingia ofisini jana tangu aapishwe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Mh. Patrick Rutabanzibwa.

WIKILEAKS YAFICHUA SIRI ZA MAREKANI…!!!

Tovuti ya Wikileaks, maarufu kwa kutetea sera za uwazi, imeanza kuchapisha mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani kuhusu viongozi wakuu duniani. Baadhi ya mawasiliano yaliochapishwa ni yale kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Marekani, pale alipopendekeza vikali kuwa Iran ishambuliwe kijeshi. Serikali ya Marekani imekashifu hatua hiyo ya kuchapisha mawasiliano hayo. Imesema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha na mabalozi wake. 

Lakini mwanzilishi wa tovuti ya Wikileaks Jullian Assange, anasema serikali ya Marekani haitaki kuwajibishwa. Wikileaks imechapisha nakala mia mbili kati ya zaidi ya laki mbili ilizonazo ya mawasiliano hayo. Hata hivyo nyaraka zote hizo zimesambazwa kwa magazeti kama vile New York Times la Marekani na The Guardian la Uingereza. 

Masuala yalioangaziwa zaidi kwenye mawasiliano hayo ni mpango wa nuklia wa Iran, ufisadi katika serikali ya Afghanistan na uhusiano kati ya serikali ya Urusi na genge la mafia. Amri ya waziri wa mambo ya nje wa marekani Hilary Clinton kuwa vigogo wa Umoja wa Mataifa akiwemo katibu mkuu achunguzwe pia imechapishwa

Sunday, November 28, 2010

SHOW YA MITINDO NITE NDANI YA FORMER MILLENNIUM NITE CLUB!

Kundi la Reggae Nite Bongamis lililotumbuiza jana live, likiwa limevalia mtindo wa kanga, kwenye show ya Mitindo nite. iliyofanyika jumamosi ya jana, Nov,27/2010 Millennium Nite Hyattsville jiji Maryland nchini marekani.

Asia Idarous. Akiwa na kundi zima la Mitundo Nite Show. Iliyofanyika jana jumamosi Nov,27/2020

Ma Winny Cassy . kanga wrap  wa kwanza kushoto,  akiwa na kundi zima la Mitundo Nite Show. Iliyofanyika jana usiku wa  jumamosi Nov,27/2020.

Ma Winny Cassy, wanamitindo wa wakuzifunga kanga  kimtindo wa gauni, bila kutumia nyuzi wala sindano. akiwakaribisha rasmi wapenzi waliohudhuria katika, Mitundo Nite usiku wa jana jumamosi Nov,272010 Hyattsville Jijini Maryland nchini marekani.

Mwanamitindo Asia Idarous, kutoka jijini Dar Es Salaam akiwakaribisha rasmi wapenzi waliohudhuria na waliomunga mkono katika show ya Mitindo nite jana jumamosi, huku akionysha vazi lake.

Hawa ndio wanamitindo  waliotupa uhondo wa ainayake jana ndani ya Bongamis Lounge Former Millennium Nite Club.


Kanga Mitindo Nite Show.













Mitindo Nite:Vazi La Kanga Wrap!

Mitindo ya kufunga  vazi la kanga kutoka kwa mtalamu. Ma Winny bila kutumia shindano, uzi, au charahani ni mikono yake anayofunga na kuwa mtindo wa gauni tosha. kutoka kwa  Ma winny kanga Fashions.

Hiyo ni kanga iliyozongwa zongwa kwa kimtindo wa gauni.