
Libya imeomba kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki ya soka na Kenya februari 9 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya football Kenya Limited Hussein Swaleh amesema Libya wako tayari kuwasili Nairobi kwa ajili ya mechi hiyo ambapo kwa sasa suala hilo linajadiliwa.
Bodi ya Utawala ya ‘Harambee Stars’ imetangaza kuwa timu yao itacheza mchezo huo ambao itauchukulia kama sehemu ya maandalizi ya mechi za kufuzu kwa michuano ya Africa Cup of Nations hapo mwezi Machi dhidi ya Angola.

No comments:
Post a Comment