Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Friday, January 28, 2011

MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI…!!!


Waziri Mkuu wa Tunisia Mohamed Ghannoushi ametangaza kufanya mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri wa serikali ya mpito, ikiwa ni moja ya njia ya kuwatuliza wananchi wanaoipinga serikali ya muda ya nchi hiyo. 

Akizungumza kwa njia ya Televisheni Waziri Mkuu huyo amesema wapambe wa rais aliyeondolewa madarakani Zine al-Abidine Ben Ali waliokuwa na nyadhfa serikali wameondolewa, huku jumla ya mawaziri 12 wakipoteza nafasi zao. Ghannouchi amesisitiza kuwa serikali anayoiongoza ni serikali ya muda na kuwa itawaongoza wananchi kuelekea katika demokrasia. Nacho Chama cha Kikuu cha Wafanyakazi cha Tunisia kinachoaminika kuhusika katika maandamano hayo kimeyaunga mkono mabadiliko ya baraza la mawaziri.

No comments:

Post a Comment