Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Saturday, January 8, 2011

MH. DR.BILAL AKITEMBELEA NDANI YAHIFADHI - MBUGA ZA WANYAMA SERENGETI…!!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal akiangalia simu yake baada ya kutumiwa ujumbe unaomkaribisha katika Jamhuri ya Kenya, wakati alipotembelea kwenye Mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama kati ya Serengeti na Loliondo leo. kulia Mama Zakia Bilal, kulia Mama Aisha Bilal.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama ya Serengeti Bw. Mtango G.G. Mtahiko, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mpaka wa Tanzania na Kenya wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo hilo liliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama kati ya Serengeti na Loliondo leo. kulia Mama Aisha Bilal, kushoto Mama Zakia Bilal.

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal wa pili kushoto na Familia yake wakiangalia Mamba na Viboko, walipotembelea moja ya Mito iliyomo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti leo. Makamu wa Rais yupo Serengeti kwa mapumziko mafupi.(Picha na Amour Nassor – VPO).

No comments:

Post a Comment