Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Saturday, January 22, 2011

MOHAMMED GHANNOUCHI WA TUNISIA AAHIDI KUJIUZULU…!!!


Waziri Mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ameahidi kujiuzulu katika wadhfa wake huo mara tu uchaguzi utakapofanyika nchini humo, wakati nchi hiyo ikielekea katika utawala wa kidemokrasia hali ambayo amesema inapaswa kutokea haraka iwezekanavyo. 

Waandamanaji nchini Tunisia wamekuwa wakidai kuondolewa kwa maafisa wote wa serikali waliokuwa wakifanya kazi wakati wa utawala wa Rais Zine El Abidine Ben Ali, aliyeikimbia nchi hiyo wiki moja iliyopita. Serikali ya mpito nchini humo ambayo inajumuisha pande zote za viongozi wa upinzani na mawaziri waliokuwa katika utawala wa Rais Ben Ali, imeidhinisha muswada utakaowezesha kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa na kuvihalalisha vyama vya siasa vilivyopigwa marufuku.

No comments:

Post a Comment