Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Saturday, January 29, 2011

NCHI YA HAITI YAPANGA TAREHE YA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI AWAMU YA KWANZA…!!!

Rais Rene Preval. 

Tume ya Uchaguzi ya Haiti imesema kuwa matokeo ya mwisho ya awamu ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini humo yatatangazwa hapo siku ya Jumatano. Tume hiyo imesema matokeo ya awali ya kura za mwezi Novemba zilizozua mvutano yatatangazwa Februari 2 mwaka huu na imepanga kuwa awamu ya pili ya uchaguzi huo itafanyika tarehe machi 20. 

Katika uchaguzi huo wa awamu ya kwanza wasimamizi wa kimataifa walisema kuwa matokeo hayo yalikuwa na udanganyifu. Awamu ya pili ya uchaguzi huo ilipaswa kufanyika wiki mbili zilizopita lakini uliahirishwa kufuatia vurugu zilizozuka nchini humo. Tume hiyo imefafanua kuwa matokeo ya mwisho ya awamu ya pili ya uchaguzi huo yatatangazwa aprili 16, 2011. 

Taarifa ya kutangazwa kwa matokeo hayo imekuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani bibi Hillary Clinton akitarajiwa kuwasili Haiti hapo kesho kwa mazungumzo na rais Rene Preval kuhusu mgogoro wa uchaguzi, ukarabati baada ya tetemeko la ardhi na kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.

No comments:

Post a Comment