Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Monday, January 10, 2011

RWANDA KUZUNGUMZIA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU…!!!


Bunge la nchini Rwanda wiki hii linatarajia kuanza mazungumzo ya wazi kuhusu jitihada za nchi hiyo katika kupunguza ongezeko la idadi ya watu na jinsi serikali itakavyoweza kuimarisha kampeni zake dhidi ya ongezeko la kasi la idadi hiyo. 

Nchi hiyo ambayo kwa sasa inaongezeko la idadi ya watu kwa asilimia 2.7 inaweza kuwa na ongezeko mara mbili la idadi hiyo kufikia mwaka 2030 iwapo hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa . Naibu spika wa Bunge la nchi hiyo Jean Damascene Ntawukuriryayo amesema ipo haja ya kubadilisha mikakati ya kudhibiti ongezeko la idadi ya watu vinginevyo jitihada za nchi hiyo kimaendeleo hazitafanikiwa. 

Ntawukuriryayo ameongeza kuwa takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Rwanda kwa sasa inashika nafasi ya 21 miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha ongezeko la watu.

No comments:

Post a Comment