JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto
Pamoja na vurugu hizo, serikali mkoani Mwanza imewataka wafanyabiashara hao kuheshimu sheria na kanuni za mipango miji zilizowekwa pia maafikiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wao, uongozi wa mkoa na halmashauri ya jiji hilo. Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa sita, zilianza saa tatu asubuhi baada ya mgambo wa jiji na askari wa kutuliza ghasia kuwatawanya wafanyabiashara hao katika maeneo ya Makoroboi, Mission na Soko Kuu.
Kutokana na hali hiyo, machinga walijikusanya na kuanza kuvamia maduka, magari kabla ya kuandamana saa 4:38 asubuhi hadi katika jengo la ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza wakishinikiza kutoondolewa katika maeneo hayo.
Nje ya jengo hilo , waliweka vizuizi vya mawe katika barabara zote zinazoingia jiji na kulazimisha pikipiki na magari yaliyokuwa yakipita kurudi yalikotoka huku wakiwa na chupa za maji ya kunawa kwa ajili ya kujikinga na moshi wa mabomu iwapo polisi wangewafyatulia mabomu ya machozi.
Soma zaid gsengo.blogspot.com/

No comments:
Post a Comment