Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Thursday, April 7, 2011

LEO NI KARUME DAY…!!!

Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe kama ya leo 7 Aprili, 1972 kwa kupigwa risasi nane na wapinga maendeleo alipokuwa Makao Makuu ya Chama cha Afro Shiraz(ASP) Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Karume aliongoza mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hapo mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa jina la Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment