Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Sunday, April 10, 2011

MAUAJI YAENDELEA SYRIA NA NIGERIA…!!!


Kundi moja la kutetea haki za binaadamu nchini Syria limesema waandamanaji 26 wamewauwa huko kusini mwa mji wa Deraa na wengine wawili katika jimbo la kati la Homs baada ya polisi kufyatua risasi kutawanya maandamano ya amani nchini humo.

Shirika la kitaifa la Haki za Binadamu nchini Syria limesema maafisa wa usalama na polisi wametawanya mikusanyiko ya amani katika mikoa kadhaa nchini humo kwa kutumia nguvu.

WAKATI HUO HUO

Watu wasiopungua wawili wameuwawa wakati wa uchaguzi wa wabunge nchini Nigeria uliogubikwa na mashambulio ya mabomu na risasi katika uchaguzi uliokuwa umeahirishwa mara mbili.

Uchaguzi wa Rais umepangwa kufanyika wiki ijayo, na utafuatiwa na uchaguzi wa magavana Aprili 26 katika majimbo 36 nchini humo.

No comments:

Post a Comment