Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Wednesday, April 20, 2011

MUSWADA WA KUONDOA SHERIA YA HALI YA HATARI WAIDHINISHWA SYRIA…!!!

          Rais Bashar al-Assad

Serikali ya Syria imeidhinisha rasimu ya mswada wa kuondoa hali ya hatari ambayo imekuwa ikitumika kwa karibu nusu karne, sheria ambayo inazuia mikusanyiko ya watu wengi pamoja na uhuru wa kutembea.

Hata hivyo pamoja na hatua hiyo ya serikali, baraza la mawaziri pia limeidhinisha sheria inayowataka wananchi wa Syria kupata kibali cha serikali ili kuandamana.

Muswada huo lazima uidhinishwe na bunge, ambalo litaanza vikao vyake mwezi ujao na hatimaye kuidhinishwa na kusainiwa na Rais Bashar al-Assad.

Waandamanaji wanaopigania demokrasia wamekuwa wakiandamana nchini Syria kwa muda wa mwezi mmoja sasa, ambapo Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International limesema kuwa vikosi vya usalama vimewaua takriban watu 200 tangu vuguvugu hilo lilipoanza.

Madai ya waandamanaji hao ni kujiuzulu kwa rais Assad na kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment