
Baraza la Usalama la Unoja wa Mataifa.
Jumuiya ya Kujihami ya NATO inayachunguza madai yaliyotolewa na askofu mmoja wa kikatoliki raia wa Italia kuwa takriban watu 40 wanaripotiwa kuuawa katika shambulio la bomu lililotokea kwenye mji mkuu wa Libya wa Tripoli.
Kulingana na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhamira ya operesheni ya kijeshi inayoendelea Libya ni kuwalinda raia wa kawaida.
Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ilichukua majukumu yake ya kusimamia operesheni hiyo.
Wakati huohuo uongozi wa Uingereza unamhoji Waziri wa mambo ya nje wa Libya Moussa Koussa aliyekimbilia huko kutafuta hifadhi baada ya kuasi na kujiuzulu.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron, amesema kuwa kitendo cha Moussa Koussa kuasi ni pigo kubwa kwa uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi.

No comments:
Post a Comment