Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Saturday, April 9, 2011

NATO YASIKITISHWA NA VIFO VYA WAASI…!!!


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Anders Fogh Rassmussen ameelezea masikitiko yake kutokana na vifo vya waasi vilivyotokana na shambulio la anga la majeshi ya jumuiya hiyo katika vifaru vya waasi nchini Libya.

Katika shambulio hilo waasi 10 waliuawa wakati ndege za NATO kwa bahati mbaya ziliposhambulia vifaru nje ya mji wa Brega.

Awali msemaji wa NATO Russ Harding alisema kuwa jumuiya hiyo haikujua kwamba waasi wamekuwa wakitumia vifaru katika operesheni zao dhidi ya vikosi vya Kanali Muammar Gadhafi.

WAKATI HUO HUO

Kundi la viongozi wa Afrika mwishoni mwa wiki hii wanatarajiwa kuitembelea Libya na kukutana na pande zote katika nchi hiyo inayoendelea kuzongwa na mgogoro kwa lengo la kutafuta haraka njia za kusitisha mapigano.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na viongozi wengine kutoka jopo la ngazi za juu la Umoja wa Afrika watakutana kwanza leo nchini Mauritania na baadae kwenda Libya kukutana na Kanali Gadhafi mjini Tripoli na viongozi wa waasi huko Benghazi kwa nia ya kumaliza mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment