
Nchi ya Ubelgiji imechukua hatua muhimu kuelekea kupiga marufuku uvaajia katika maeneo ya umma wa vazi linalovaliwa na Waislamu linalofunika mwili mzima linalojulikana kama ‘Burqa’.
Bunge la nchi hiyo limeunga mkono kwa wingi hatua hiyo, lakini Baraza la Seneti bado lina wiki kadhaa za kuamua iwapo liupeleke mswada huo kujadiliwa zaidi na kuupigia kura.
Mwaka jana Bunge la Ubelgiji lilikaribia kuidhinisha hatua kama hiyo, lakini hatua hizo zilisitishwa katika dakika za mwisho wakati muungano unaounda serikali ya nchi hiyo ulipovunjika.
Iwapo mswada huo utapitishwa, Ubelgiji itakuwa nchi ya pili katika bara la Ulaya kupiga marufuku vazi hilo linalofunika uso, baada ya Ufaransa kupitisha marufuku hiyo Septemba mwaka jana.

No comments:
Post a Comment