
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Meja Jenerali Kale Kaliyihura.
Na.MO BLOG TEAM
Kumekuwepo taarifa kuwa magaidi wa kundi la Al-Shabaab la Somalia wanampango wa kufanya shambulio la kigaidi nchini Uganda katika kipindi hiki cha siku kuu ya Pasaka.
Kundi hilo linalohusishwa na kundi la kigaidi duniani linaloongozwa na Osama Bin Laden la Al-Qaeda, tayari limedai kuhusika na shambulio la mabonu lililopoteza maisha ya watu zaidi ya 70 nchini Uganda katika viwanja vya mchezo wa Rugby vya Kyadondo na Ethiopian Village jijini Kampala mnamo Julai 11 mwaka jana.
Akitoa taarifa ya mwaka ya Uhalifu na Usalama Barabarani nchini humo Mkuu wa Jeshi la Polisi Meja Jenerali Kale Kaliyihura amesema jeshi hilo linafanya kila jitihada kuzuia uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi hayo, na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

No comments:
Post a Comment