Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Thursday, June 16, 2011

ALBASHIR AKACHA MKUTANO WA UCHUMI MALAYSIA…!!!


Rais Omar al-Bashir wa Sudan ambaye anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika jimbo la Darfur , hatahudhuria jukwaa la kiuchumi litakalifanyika wiki ijayo nchini Malaysia.

Rais al Bashir alialikwa kuhudhuria jukwaa hilo la kiuchumi la viongozi wa Asia na Afrika la siku tatu, ambalo litaanza siku ya Jumapili mjini Putrajaya, ambapo mpango wake huo wa kushiriki alilaumiwa vikali na mashirika ya haki za binadamu.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Malysia Anifah Aman ameiambia televisheni ya taifa ya Bernama kwamba Rais al Bashir hatahudhuria mkutano huo kutokana na kile alichoelezea “hali isiyotazamiwa” na badala yake atamtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje.

Malaysia haijasaini makubaliano ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya ICC, ambayo wanachama wake wanashurutishwa kumkamata Al Bashir iwapo ataingia katika ardhi za nchi zao.

Wakati huohuo Rais huyo wa Sudan anatarajiwa kufanya ziara nchini China baadaye mwezi huu.

Hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

No comments:

Post a Comment