Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Tuesday, July 5, 2011

CHEVEZ ARUDI NYUMBANI BAADA YA MATIBABU…!!!


Rais wa Venezuella Hugo Chevez akisalimia wananchi wake baada ya kurejea nchini akitokea nchini Cuba kwenye matibabu ya Saratani.

Rais Hugo Chaves wa Venezuela amerejea nyumbani kutoka Cuba ambako alikuwa akipata matibabu ya saratani kwa karibu mwezi mmoja.

Akizungumza na maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika nje ya makaazi ya rais mjini Caracas, Rais Chavez amesema yuko tayari kupambana na matatizo ya afya yake.

Akiwa amevalia sare za jeshi na kuonekana mwenye afya njema, Rais Chavez alikiri kuwa alikuwa mgonjwa sana na kuelezea kwamba kupona kwake ni kama miujiza.

Lakini hata hivyo ameonya kuchukua tahadhari juu ya afya yake hiyo.

No comments:

Post a Comment