
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu.
Uturuki imeliunga mkono Baraza la taifa la mpito, kundi la waasi wa Libya linalopambana kumng’oa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.
Katika ziara yake aliyoifanya katika mji wa Benghazi ulio ngome ya waasi, Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema baraza hilo ni wawakilishi halali wa watu wa Libya.
Wakati huohuo waasi wa Libya wameonyesha matumaini yao juu ya mustakabali wa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Waziri wa zamani wa sheria na kiongozi wa waasi Mustafa Abdel Jalil amesema Gaddafi anaweza akabakia katika nchi hiyo, iwapo atakubali kujiuzulu.
Lakini hata hivyo mmoja wa wasaidizi wa kiongozi huyo wa waasi amepinga kuwepo uwezekano huo.

No comments:
Post a Comment