Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Thursday, November 3, 2011

Wacongoman watarajiwa kuzidi kukimbilia Uganda kabla ya uchaguzi mkuu

Na Leyla Ndinda, Kampala
Siku chache tu baada ya kampeni za uchaguzi mkuu kuanza rasmi nchini Congo shirika la kuyashughulikia maslahi ya wakimbizi nchini Uganda- UNHCR imethibitisha kuwapokea wakimbizi zaidi ya elfu moja wa kutoka Congo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kwa mujibu wa VOA wakimbizi wa Congo wamekimbilia Uganda wakisema maisha yao yako hatarini kwa sababu mara kwa mara wanashambuliwa na majambazi ingawa hawaweza kuwatambua majambazi hawa ni akina nani na wanatoka wapi. Kusoma zaidi bofya

Kambi ya Kyangwali ina wakimbizi elfu ishirini na nne, huku wakimbizi elfu ishirini kati ya hawa wakitoka Congo na idadi yao ikizidi kuongezeka kwa mujibu wa twakimu za UNHCR.

Kamanda wa Polisi wa Kambi ya Kyangwali Taseburwa Kirya amesema ameshapokea wakimbizi mia saba ishirini n nane kutoka Congo kuanzia mwezi wa nane mwaka huu kufikia sasa.

Idadi hii ni ya wakimbizi ambao wamehakikiwa na UNHCR ili kuhakikisha kuwa ni wakimbizi na sio raia wa Uganda wanaodai ni wakimbizi ili wapate msaada. Zoezi la kuwahakiki watu waliokimbilia pale kambini lingali linaendelea kwa hivyo idadi ya wakimbizi kutoka Congo yaweza kuongezeka. Kamanda Taseburwa Amos anasema ni muhimu kuwahakiki wakimbizi ili

Kuthibitisha kama wao ni wakongomani kwa sababu kuna watu ambao hawana mashamba ya kulima kwa hivyo wanakuja hapa kusajiliwa kama wakimbizi ili wapewe shamba la kulima. Pia tunavyo vitu vingine tunavyowapa wakimbizi kama chakula na madawa kwa hivyo waganda wanataka kusajiliwa ili nao wafaidike.

Afisa wa mawasiliano wa UNHCR nchini Uganda Needa Jehu- Hoya anasema wanatarajia wakongomani wengi kukimbilia Uganda kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wakiogopa huenda kukazuka vita wakati na baada ya uchaguzi. Endelea kusoma Sundayshomari

No comments:

Post a Comment