
Baada ya mozozo wa muda mrefu kuhusu mauaji yanayohusishwa na almasi katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Zimbabwe almasi za nchi hiyo zilikwama na kukosa wateja kwa kuwekewa vikwazo.
Lakini hatimaye hayo yamewekwa nyuma kwenye ukurasa wa historia ya Zimbabwe Sauti ya Amerika inaripoti kuwa Zimbabwe imefikia makubaliano ya kuuza almasi zake zilizochimbwa katika mgodi wenye mzozo wa Marange. Kusoma zaidi bofya
Baraza la almasi duniani lilisema makubaliano hayo yalifikiwa jumanne kwenye mkutano katika mji mkuu wa Congo Kinshasa. Iliidhinishwa na wanachama wa Kimberly Process mpango uliowekwa kuzuia kile kilichoitwa almasi za damu kufikia masoko ya kimataifa .
Makubaliano hayo yanaruhusu migodi miwili ya Marange kuuza almasi kwenye soko la kimataifa. Mgodi wa tatu ulioendeshwa na kampuni ya wachina ya Angin , utaruhusiwa kuanza tena mauzo kufuatia kupitishwa na wasimamizi wa Kimberly. Endelea kusoma sundayshomari.com

No comments:
Post a Comment