Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Monday, January 31, 2011

Add caption

SUN., JANUARY 30: NFL Pro Bowl Day!!

Probowl

TIMU YA LIVERPOOL YAKUBALI MKATABA WA £23M KUMSAJILI LUIS SUAREZ…!!!


Klabu ya Liverpool ya Uingereza imekubali kutoa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 23 ili kumsajili mshambuliaji Luis Suarez kutoka klabu ya uholanzi ya Ajax Amsterdam. 

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 24 amefaulu majaribio ya afya, huku kukamilika kwa uhamisho wake kukitarajiwa kukamilika hivi leo. Hapo awali Liverpool ilitoa ofa ya paundi milioni 12.7 kwa ajili ya Suarez, lakini klabu ya Ajax ikawataka kuongeza ofa hiyo ili kuwashawishi wadachi hao kuumuza mshambuliaji huyo.

Fulham Yatoka Mikono Juu Kwa Kuwatwanga Tottenham 4-0


MATOKEO YA MICHEZO MINGINE.

Aston Villa 3-1 Blackburn Birmingham 3-2 Coventry Burnley 3-1 Burton Albion Stevenage 1-2 Reading Sheffield Weds 4-1 Hereford Bolton 0-0 Wigan Arsenal 2-1 Huddersfield West Ham 3-2 Nottingham Forest Wolves 0-1 Stoke Southampton 1-2 Man Utd

RATIBA YA HATUIA YA TANO;

West Ham v Burnley Notts County or Man City v Aston Villa Stoke City v Brighton Birmingham City v Sheff Wed Leyton Orient v Arsenal Everton or Chelsea v Reading Man Utd v Crawley Fulham v Bolton or Wigan Michezo hii wa hatua ya tano ya kombe la FA imepangwa kuchezwa Februari 19/20 mwaka huu.

NCHINI NIGERIA ISSOUFOU, OUMAROU NA AMADOU WAWANIA URAIS NIGER…!!!


Bw.Seini Oumarou mmoja wa wagombea Uraisi nchini Niger.

Kumekuwa na mistari mirefu katika vituo vya kupigia kura nchini Niger katika uchaguzi wa kwanza wa rais tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa Mamadou Tadja mwaka mmoja uliopita. Taarifa zinasema kumekuwa na hali ya utulivu katika mji mkuu wa Niamey huku mambo yakionekana kuwa shwari sambamba na kuwekwa kwa ulinzi mkali. 

Wagombea wa nafasi hiyo akiwemo Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini humo Mahamadou Issouf na Waziri Mkuu wa zamani Seini Oumarou na Hama Amadou wanaonekana kuwa na wafuasi wengi. Kiongozi aliyepinduliwa Tadja aliondolewa madarakani baada ya kupingwa kwa kiasi kikubwa kwa kutaka kuongoza tena kwa awamu ya tatu. Mapema mwezi huu kiongozi huyo alitolewa katika kizuizi cha nyumbani na kupelekwa gerezani na kutuhumiwa kwa rushwa.

Mkutano Wa Watanzania Wa Washington DC (DMV)

Mh. Balozi Mwanaidi Maajar akijitambulisha rasmi kwa watanzania waliojitokeza states mbali mbali, pamoja na watanzania wanaoishi hapa washington DC,

Na Sunday Shomari

Mkutano uliofajika jiji hapa siku ya jumamosi Jan, /29/2011 Mh. Balozi Mwanaidi Maajar.  Mambo mengine alitoa nafasi ya watanzania hao kuweza kwenda kumwona ofisini kwake kila Jumanne na kufanikisha uchaguzi wa kamati ya katiba ya jumuiya ya watanzania. Aidha mh. Balozi pia aliwapa nafasi maafisa wake wa ubalozi kujitambulisha kwa watanzania na pia kutoa mawasiliano yao wazi ikiwemo simu na barua pepe na kuweka bayana kuwa milango ya mawasiliano kati ya ubalozi na watanzania iko wazi. 

Balozi pia alikuwa wa kwanza kutoa mawasiliano yake wazi mbele ya watanzania wa Washington Dc ikiwemo mpaka nambari yake ya mkononi kitu ambacho hakijawahi kuonekana kwa viongozi wengine waliopita katika ofisi yake. (Mpiga picha wetu swahilivilla)

Kwa kazi nzuri aliyoifanya mzee wa Changamoto yetu  kijana anaestahili sifa zote katika web edit Mubelwa Bandio akisalimiana na Mh. Balozi Mwanaidi Maajar katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mahali Hollywood Ballroom ndani ya Silver spring jijini Maryland nchini marekani. Kwa wale wasiosikia mkutano huu usikose kumtembelea Changamotoyetu.blogspot.com/

Ebou waswahilivilla akiwa bega kwa bega na anko Sunday Shomari katika mambo ya kunasa image za waliohudhurika katika mkutano, uliomalizika kwa mafanikio makuwa ya kuchagua viongozi wa jumuiya ya watanzania wanaoishi jijini hapa. Usikose kutembelea libeneke la Sunday Shomari kwa kusoma habari za kilasimu. Gonga hapa Sundayshomar.

Maalim Seif Ameir akiwakilisha shirika  la utali, Cultural Toursim ndani ya nchi yetu kamavile mlima wa kilimanjaro, kisiwa cha zanzibar na serengeti, kukaribisha watalii wakaone wanyama kule nyumbani tanzania.

JK. Prof. Julius Nyang'oro Kuhudhuria Kwenye Mkutano!


Ebou Shatry web edit wa swahilivilla akipata sign kutoka kwa muandishi wa kitabu cha wasifu wa JK. Prof. Julius Nyang'oro, katika mkutano rasmi wa Mh. Balozi Mwanaidi Maajar, kujitambulisha rasmi kwa wa tanzania wanaoishi  Washington DC Metro. siku ya jumamosi Jan 29/2011

Didi Vava  pia alionyesha uzalendo wakuhudhuria katika mkotano wetu.


Tumuangalini sana Kiongozi tunaemtarijia wa kizazi kimpya Londa Fazil Londa. pia alikuwepo katika mkutano.

Dmk Dmkglobal


Pia alionyesha uzalendo nakuhudhuria  katika mkotano

WAANDAMANA SUDAN…!!!


Polisi nchini Sudan wamepambana na wanafunzi katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum, katika maandamano ya kuipinga serikali licha ya ulinzi mkali uliopo. Watu kadhaa walikamatwa na polisi wakati wa maandamano hayo. 

Chama cha upinzani nchini humo cha Umma kimetangaza majina ya watu 40 waliokamatwa kuhusiana na maandamano hayo. Mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa ni vijana walikuwa wakitoa wito wa kutaka mabadiliko katika utawala.

Dramatic video as thousands clash with Egypt riot police in Cairo

BAADHI YA WAANDAMANAJI MISRI WAKIUKA AMRI ZA SERIKALI…!!!


Polisi nchini Misri wameamriwa kurejea mitaani katika mji wa Cairo huku amri ya kutotembea usiku ikiongezwa muda huku rais wa nchi hiyo akijaribu kutafuta muafaka nchini humo. 

Pamoja na polisi kurejea kuranda mitaani lakini waandamanaji wameendelea kupiga kambi katika mitaa ya Cairo na kutoa wito wa kufanya maandamano ya nchi nzima hii leo huku wakimtaka rais Hosni Mubarak kuachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 30. Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imesoma barua ambayo rais wa nchi hiyo amemuandikia Waziri Mkuu mpya Bw. Ahmed Shafiq ambapo amemtaka kuharakisha mabadiliko ya kisiasa na umuhimu wa kuwepo mabadiliko ya katiba na bunge. 

Pia rais huyo ametoa wito wa kuwekwa kwa sera za kiuchumi yatakayoshughulikia matatizo ya wananchi na kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa kutengeneza nafasi za kazi. Wakati huo huo upinzani nchini Misri umesema umekubaliana kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Mohamed El Baradei kuongoza ujumbe wa majadiliano kati yao na serikali. 

Muungano wa vyama kwa ajili ya kuleta mabadiliko nchini humo, ambao unajumuisha vyama mbalimbali vya upinzani, kikiwemo kile kilichopigwa marufuku cha undugu wa kiislamu -Muslim Brotherhood-, vimempendekeza Bw. El Baradei, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.

MKUTANO WA MARAIS NA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI ADDIS ABABA


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 21 wa Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika mjini Addis Ababa.

Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Ghana Mheshimiwa Jerry Rawlings wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 30.1.2011.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa tarehe 30.1.2011 (Picha zote na John Lukuwi).

VIJIMAMBO YA TIMIZA MWAKA TANGU KUVUMBULEWA KWAKE.!


Sunday, January 30, 2011

CHEKA UNENEPE SASA HA HAHA.

WAREMBO WA TANZANIA KUSURA WAKINGIA KAMBINI LEO HII..!!

WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini leo katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili. Mchakato wa kuwapata wasichana hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa, Mbeya na Ruvuma. 

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo View Resort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa. Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la. “Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema. 

Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera), Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora). Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es Salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma). 

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao. Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

TANZANIA PRESIDENT DR. KIKWETE IN ADDIS FOR THE AFRICAN UNION SUMMIT…!!!

President Dr. Jakaya Kikwete shake hands with President Dr. Bingu Mutharika of Malawi shortly after opening 16th ordinary Session of the Assembly of the African Union at Addis Abba Ethiopia this afternoon.

President Kikwete flew in Addis last night from Davos Switzerland after attending the World Economic Forum (WEF) 2011 where he launched a strategy to significantly increase food production while conserving environmental resources and spurring economic growth in Tanzania.

Others in the picture are from left front row Liberia’s President Sirleaf Johnson, The chairman of the AU Commission Jena Ping and right is the United Nation Secretary Ban-ki-Moon (Photo by Freddy Maro)

Watanzania Wa Washington DC (DMV) Wafanikiwa Kuunda Jumuiya Na Kuchagua Viongozi Wampito

Mh. Balozi Mwanaidi Maajar akijitambulisha rasmi kwa watanzania waliojitokeza states mbali mbali, pamoka na watanzania wanaoishi hapa washington DC,

Watanzania mbali mbali waliohudhurika katika mkutano wa Mh. Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.

Mh. Balozi Mwanaidi Maajar (Katikati) akiwa na Viongozi waliochaguliwa kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro. Ndio hawa hapa mnaowa waona katika picha. (Picha  swahilivilla.)

NCHI YA MAREKANI YAIPIGA JEKI TANZANIA KUENDELEZA KILIMO KUSINI MWA NCHI…!!


Serikali ya Marekani ya Rais Barack Obama juzi, Ijumaa, Januari 28, 2011, ilitangaza kuwa inatoa kiasi cha dola za Marekani milioni mbili (sawa na zaidi ya sh bilioni mbili) kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wa Mradi wa Uendelezaji Kilimo Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT). 

Hatua hiyo ya Serikali ya Marekani ambayo kwa pamoja na Serikali za Tanzania na Vietnam inasaidia kusukuma utekelezaji wa mipango mipya ya kuboresha kilimo katika Tanzania na Vietnam, chini ya visheni mpya ya “A New Vision for Agriculture”, ni moja ya hatua nyingi zilizochukuliwa na Serikali hiyo kuunga mkono jitihada za Tanzania kufanikisha Mradi huo. Mchango huo mkubwa wa Marekani ulitangazwa jana na Mtendaji Mkuu na Mtawala wa Mfuko wa Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa wa Marekani (USAID) Dkt. Rajiv Shah wakati alipoungana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuutangaza Mradi huo kwenye mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari mjini Davos, Uswisi. 

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari ambako Dr. Shah pamoja na viongozi wengine wakuu wa mashirika makuu ya kibiashara 17 duniani wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi huo waliunga na Rais Kikwete, kiongozi huyo wa USAID alitangaza: “Tunakushukuru Rais Kikwete kwa kutushirikisha katika mkutano huu wa kwako na waandishi wa habari hasa wakati huo ambako bei za vyakula duniani zinaonyesha dalili za kuanza kupanda tena. Marekani inayo kila dhamira ya kuunga mkono Mradi huu ili uweze kufanikiwa na kufikia malengo yake,” alisema Dkt. Shah na kuongeza: 

“Ili kuonyesha dhamira ya Serikali ya Marekani katika kuunga mkono Mradi huu, ninayo furaha ya kutangaza mchango wa nyongeza wa Marekani katika mfuko wa uwezeshaji wa Mradi huu wa kiasi cha dola za Marekani milioni mbili.” Tanzania inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 50 kama mfuko wa kuanzisha SAGCOT ambayo uwekezaji wake unatarajiwa kufikia kiasi cha sola za Marekani bilioni 3.4 katika miaka 20 ijayo. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mkoa ongozi katika kilimo cha chakila ambayo ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma. 

Mshiriki mwingine kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Hugh Grant ambaye ni Mwenyekiti, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mansanto ya Marekani inayojihusisha na kilimo duniani alisema kuwa mpango huo wa kilimo katika Tanzania na Vietnam utatumia mbegu za asili katika nchi hizo na siyo mbegu zilizotengenezwa kisayansi za GMO. “Kwa sasa mipango yetu ni kutumia mbegu za jadi katika nchi hizo mbili – mbegu za asili, mbegu safi, mbegu zinazoweza kuhimili magonjwa na wadudu katika nchi hizi mbili. Hizi ndiyo mbegu zinazoweza kuwa za maana katika Mradi huu.“ Grant aliwaambia waandishi wa habari. 

Kuhusu uwezekano wa makampuni 17 ya kimataifa yanayoshiriki katika kufanikisha Mradi huu kupanga bei za mazao yatakayozalishwa chini ya Mradi huu, Rais Kikwete aliwaambia waandishi wa habari: “Kiasi kikubwa cha mazao kitakachozalishwa chini ya Mradi huu kitakuwa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata chakula cha kutosha. Kama kuna ziada, basi bei za mazao hayo ya ziada, zitaamuliwa na kiwango cha bei kwenye soko la kimataifa.” Naye Paul Polman, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever katika Uingereza alisema kuwa mazao yatayozaliwa katika Tanzania chini ya Mradi huu yatakuwa na soko kubwa ndani na nje ya Tanzania. “Kuna mahitaji makubwa ya chakula duniani. Baadhi ya watu wanaishi kwa kutegemea kiasi kisichofikia dola moja ya Marekani kwa siku. 

Kuna watu wanatumia kiasi cha asilimia 70 ama 80 cha kipato chao kununua chakula. Lazima dunia izalishe chakula zaidi kwa sababu dunia isiyokuwa na chakula cha kutosha itakuwa ni dunia isiyokalika.” Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari wa kimataifa, Rais Kikwete alikutana na kuwa na mazungumzo na Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Andrew ambaye ni mwakilishi maalum wa Uingereza kuhusu masuala ya biashara ya kimataifa na uwekezaji. Katika mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumzia nafasi za Uingereza kuwekeza katika Tanzania na jinsi Tanzania inavyoweza kuwekeza katika uchumi wa Uingereza kama inataka na inao uwezo huo. Baadaye jioni ya jana, Rais Kikwete alikutana na Waziri Mkuu wa Norway, Mheshimiwa Jens Stoltenberg na pia kukutana na Bwana na Bibi Bergman ambao wamekuwa wasaidia huduma za afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hasa Kitengo cha Tiba ya Meno. 

Kabla ya kuondoka mjini Davos kwenda Addis Ababa, Ethiopia leo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika, Rais Kikwete alikuwa na mfululizo wa mikutano kwenye Hoteli ya Sheraton ya mjini Davos alipokuwa amefikia. Rais Kikwete amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Accenture Development Partnership, Bwana Gib Bulloch kujadili jinsi gani teknolojia ya kisasa ya habari inavyoweza kutumika katika ufundishaji wa masomo katika shule za Tanzania. Rais pia amekutana na kuzungumza na Bwana John Davies, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Intel anayeshughulikia na masoko na pia amekutana na Dkt. 

Nkosana Moyo, Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kuzungumzia jinsi gani benki hiyo inavyoweza kuchangia maendeleo ya SAGCOT. Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Bwana Richard T Clark, Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Dawa ya Merck ambako mazungumzo yaliyohusu kuhusu maandalizi ya kupatikana kwa dawa ya kuwezesha chanjo ya kinga la kansa ya shingo ya kizazi dhidi ya akinamama wa Tanzania iliyopangwa kuanza mwaka ujao.

WAMACHINGA WALETA KIZAZA MKOWANI MWANZA

JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto

 
Pamoja na vurugu hizo, serikali mkoani Mwanza imewataka wafanyabiashara hao kuheshimu sheria na kanuni za mipango miji zilizowekwa pia maafikiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wao, uongozi wa mkoa na halmashauri ya jiji hilo.  Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa sita, zilianza saa tatu asubuhi baada ya mgambo wa jiji na askari wa kutuliza ghasia kuwatawanya wafanyabiashara hao katika maeneo ya Makoroboi, Mission na Soko Kuu.

Kutokana na hali hiyo, machinga walijikusanya na kuanza kuvamia maduka, magari kabla ya kuandamana saa 4:38 asubuhi hadi katika jengo la ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza wakishinikiza kutoondolewa katika maeneo hayo. Nje ya jengo hilo , waliweka vizuizi vya mawe katika barabara zote zinazoingia jiji na kulazimisha pikipiki na magari yaliyokuwa yakipita kurudi yalikotoka huku wakiwa na chupa za maji ya kunawa kwa ajili ya kujikinga na moshi wa mabomu iwapo polisi wangewafyatulia mabomu ya machozi.

DK. MOHAMED GHARIB BILAL AKIWA NA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA TAASISI YA TEKNOLOJIA YA DAR ES SALAAM LEO..!!!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitunuku Shahada, Stashahada na Vyeti kwa wahitimu 445 katika ngazi ya Uhandisi Kompyuta, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Uhandisi Elektronik, Mawasiliano ya Anga, Uhandisi wa Mitambo ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara kwenye Mahafali ya Nne ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salaam. Kulia Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa J.W.A.Kondoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza Mwanafuzi J. Mgaya Mhitimu Bora kwa mwaka 2010- 2011 katika Taasisi ya Teknologia ya Dar es salaam kwenye mahafali ya nne ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salaam, ambapo jumla ya Wahitimu 445 katika ngazi za Uhandisi Kompyuta, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Uhandisi Elektronik, Mawasiliano ya anga, Mitambo ya sayansi naTeknolojia na Maabara walitunukiwa Shahada Stashahada na Vyeti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiongoza maandamano ya wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam katika Mahafali ya nne ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salamm. Kwenye Mahafali hayo Jumla ya wahitimu 445 wa ngazi mbalimbali walitunukiwa Shahada, Stashahada na Vyeti. Kushoto Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa J.W.A. Kondoro, kulia Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Profesa Mshoro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa wa pili kushoto, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia wa Dar salaam Profesa J.W.A Kondoro kushoto, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Profesa Mshoro, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya nne ya kutunuku Shahada Stashahada na Vyeti, yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Dar es salaam

Saturday, January 29, 2011

Wimbo Wa Chori Chori Tarab..!!!

TONITE IT'S ALL ABOUT AQUARIUS BRITHDAY BASH @ MILLENIUM..BEST PLACE TO BE IN THE D.M.V..EARLY ARRIVAL STRONGLY SUGGESTED!

Add caption

Cheka unenepe Na Tyler Perrys House of Payne.!

POLISI UGANDA WALAZIMIKA KUMSINDIKIZA MCHUNGAJI…!!!


Polisi nchini Uganda wamelazimika kumsindikiza mchungaji aliyetoa mahubiri katika mazishi ya aliyekuwa mwanaharakati wa haki za mashoga nchini Uganda David Kato, baada ya kuwaambia watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga watubu, hali iliyozua mtafaruku. 

Mchungaji huyo wa kanisa la Anglikana Thomas Musoke katika mahubiri yake aliwaambia waombolezaji kuwa vitendo vya kishoga ni vitendo vya kishetani. Mamia ya watu walikusanyika katika mazishi ya mwanaharakati huyo aliyefariki baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana, yaliyofanyika kijijini kwake karibu na mji mkuu wa Kampala Wanachama wenzake wa kundi la Sexual Minorities in Uganda (Smug)wamesema marehemu Kato alikuwa akipokea vitisho vya kuuawa tangu jina, picha na anuani ya anapoishi vilipochapishwa kwenye gazeti moja la nchini humo mwaka uliopita. 

Vitendo vya kishoga ni kinyume cha sheria nchini Uganda, na adhabu yake hufikia hadi kifungo cha miaka 14 gerezani, ambapo siku za karibuni mbunge mmoja nchini humo alitaka adhabu hiyo kuongezwa hadi kufikia adhabu ya kifo kwa baadhi ya mazingira.

MADIRA NA MITANDIO YAKE SASA YANAPATIKANA JIJINI HAPA.!




Kwa wale wanaopenda kujitanafasi. katika mitindo ya kujimwaga, napenda kuwajulisha rasmi, tumepokea Mali mpyaa. Nguo za madira na mitandio yake. Bei yake ni ya wastani. ukilinganisha na yamadukani. Bila ya kupoteza muda. haraka iwezekanavyo. Tusije Tukalaumiana, kwa mwenye kupenda akakosa raha za kujitanafsi. wasiliana nasi kwa number ya simu (301)728-3977 

LEO NI MKUTANO KWA WATANZANIA WA NAOISHI DMV

Tangazo  lamkutano kwa watanzania wote waishio Washington DC Metro(DMV) Mnakaribishwa Nyote, katika mkutano rasmi wa watanzania. Madhumuni ya mkutano huo yatakuwa yafuatayo:-

(i) Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.

(ii) Kuchagua na kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya jumuiya na hatimaye kuitisha na kusimamia uchaguzi mkuu wa Jumuiya mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro.

(iii) Masuala mengineyo muhimu yatakayojitokeza yanayohusu watanzania waishio hapa Washington DC Metro. RATIBA YA MKUTANO:

LEO JUMAMOSI TAREHE  29, 2011 MAHALI: Hollywood Ballroom - 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring-MD 20906 (Sehemu ya maegesho ipo yakutosha) MUDA: Saa 10.30 jioni (Tafadhali zingatia muda) Ahsanteni

NI NANI ATAKAEKUWA MWENYEJI WA CAN 2015 NA 2017.


 Fumbo la nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mataifa bara la Afrika za mwaka 2015 na 2017 kati ya nchi za Afrika kusini pamoja na Morocco litafumbuliwa kesho baada ya kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kitakachofanyika mjini Lubumbashi huko Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo. 

Kikao hicho kinaketi hiyo kesho huku nchi hizo mbili zikiwa nchi pekee zilizowasilisha maombi ya kuwa wenyeji wa fainali hizo za mwaka 2015 ambapo hata hivyo kila nchi inatamani kuwa mwenyeji wa fainali za mwaka huo na si mwaka 2017. Raisi wa chama cha soka nchini Afrika Kusini Kirsten Nematandani tayari ameshatangaza azma yao ya kutaka kuona wanashinda nafasi ya kuandaa fainali za mwaka 2015 hivyo wana imani wajumbe wa CAF wataipa nafasi kubwa nchi yao kutimiza malengo waliyojiwekea. 

Amesema hatua ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 haitoleta chachu nzuri kwa nchi kama Afrika kusini ambayo bado ipo kwenye heka heka za kushuhudia fainali kubwa za soka zikiunguruma katika radhi ya nchi hizo mara baada ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010. Kwa upande wao Morocco nao wanaitaka nafasi hiyo ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2015, ili kuiwezesha nchi yao kujitangaza zaidi baada ya kufifia katika medani ya soka la barani Afrika sambamba na lile la ulimwengu mzima. 

Yoyote atakaetangazwa kuwa mshindi katika fainali za mwaka 2015 hiyo kesho, atamfanya mpinzani wake kusubiri hadi mwaka 2017 ili aweze kuwa mwenyeji wa fainali za mwaka huo. Ikumbukwe kuwa fainali za mataifa ya bara la Afrika kwa mwaka 2012 zimepangwa kufanyika Equatorial Guinea kwa kushirikiana na nchi ya Gabon, zikifuatiwa na fainali za mwaka 2013 zitakazofanyika nchini Libya. 

Kikao hicho cha kamati ya utendaji ya CAF kitafanyika mjini Lubumbashi saa chache kabla ya kuachezwa kwa mchezo wa kuwania ubingwa wa Super Cup ambapo mabingwa wa soka barani Afrika TP Mzembe watapambana na mabingwa wa kombe la shirikisho FUS Rabat.

I AM HERE TO GET YOUR JOB DONE

Fireplace With Ceramic tile





Welcome to Abou's tile Contractors http://fundiujenzi.blogspot.com I've been a local custom tile installer in the Washington Dc Maryland and Virginia area for the past 7 years, I take pride in my work and take special care to make it just (perfect) for you. 

 If you are looking for professional tile installer for your project you have came to the right place, Please look around the blog for more information and to see pictures of tile projects that I've done. If you need a bid on your tile project please contact me and I would love to help you with your ideas and give you a free estimate. Abou's Contractors - 301-728-3977.

Kitchen Designs with Worth Modern Appliances

Picture of Charming Kitchen Design Furniture and Decoration suitable foe Luxury Home Architecture
These are the modern kitchen appliance pictures that can become the references in furnishing your kitchen rooms.

In the pictures above, you can see the elegant interior design and decorating idea that is very good to be the kitchen interior decorating model for your kitchen room. The pictures below are the modern appliances that can become the alternatives in completing your kitchen with modern luxury appliances.

NCHI YA HAITI YAPANGA TAREHE YA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI AWAMU YA KWANZA…!!!

Rais Rene Preval. 

Tume ya Uchaguzi ya Haiti imesema kuwa matokeo ya mwisho ya awamu ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini humo yatatangazwa hapo siku ya Jumatano. Tume hiyo imesema matokeo ya awali ya kura za mwezi Novemba zilizozua mvutano yatatangazwa Februari 2 mwaka huu na imepanga kuwa awamu ya pili ya uchaguzi huo itafanyika tarehe machi 20. 

Katika uchaguzi huo wa awamu ya kwanza wasimamizi wa kimataifa walisema kuwa matokeo hayo yalikuwa na udanganyifu. Awamu ya pili ya uchaguzi huo ilipaswa kufanyika wiki mbili zilizopita lakini uliahirishwa kufuatia vurugu zilizozuka nchini humo. Tume hiyo imefafanua kuwa matokeo ya mwisho ya awamu ya pili ya uchaguzi huo yatatangazwa aprili 16, 2011. 

Taarifa ya kutangazwa kwa matokeo hayo imekuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani bibi Hillary Clinton akitarajiwa kuwasili Haiti hapo kesho kwa mazungumzo na rais Rene Preval kuhusu mgogoro wa uchaguzi, ukarabati baada ya tetemeko la ardhi na kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Washington DC Pepco: "Working as Hard as We Can to Restore Service"

View more news videos at: http://www.nbcwashington.com/video.

Muammar Gaddafi Ameunga mkono Kenya Na Kusheriki Kamati Ya Uhalafu (ICC)


Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ameunga mkono nia ya Kenya ya kuahirisha kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) inayowakabili watuhumiwa sita wa Kenya waliotajwa katika orodha ya Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno ocampo. 

Gaddafiamesema Kenya ni mshirika muhimu katika taasisi za kimataifa kama vile umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, hivyo maoni ya nchi hiyo ya namna ya kukabiliana na masuala yake ya ndani lazima yaheshimike. Rais huyo wa Libya amesema imetoka mbali katika kuheshimu haki za binadamu, na iwapo Kenya imesema inataka kutumia taratibu za kimahakama za ndani ya nchi kushughulikia suala la watuhumiwa wa vurugu za mara baada ya uchaguzi basi ikubaliwe. 

Rais Gaddafi amesema hayo alipokutana na Makamu wa rais wa Kenya Kalonzo Musyoka nje ya mji wa Tripol, ambapo aliongeza kusema kuwa matatizo ya Afrika yanahitaji utatuzi wa kiafrika. Amesema bara la Afrika linapaswa kuhuitaji usaidizi wa kimataifa pale tu mataifa ya afrika yatakaposhindwa kusimamia na kutatua masuala yao ya ndani.

VIDEO NI VURUGU ZA WA EGYPT NDANI YA MJI WA CAIRO.!

Rais Hosni Mubarak wa Misri Amevunja Baraza La Mawaziri.!!


Rais Hosni Mubarak wa Misri amelivunja baraza la mawaziri wa serikali yake na na kutetea wajibu wa vikosi vya majeshi ya ulinzi nchini humo kwa kuwadhibiti waandamanaji wanaoipinga serikali. 

Rais huyo ametoa wito wa kufanyika kwa majadiliano ya kitaifa ili kuzuia vurugu, baada ya kuzuka mapambano kati ya polisi na waandamanaji wanaolalamika kuhusu umaskini na utawala wa kidikteta. Katika kauli yake ya kwanza tangu kuzuka kwa maandamano hayo katika miji ya Cairo, Alexandria na Suez ambayo takriban watu 26 wamekufa huku mamia wakijeruahiwa, rais Mubarak pia amesema baraza jipya la mawaziri linatarajiwa kutangazwa leo. 

Machafuko hayo yamewashutusha wengi katika eneo la Mashariki ya Kati ambako viongozi wengine wa kiimla, huenda wakakabiliwa na changamoto na mtikisiko katika masoko ya kimataifa. Muda mfupi baada ya rais Mubarak kutoa hotuba yake, waandamanaji walirejea barabarani kwa wingi licha ya kutangazwa amri ya kutotoka nje.

NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA YAFANYIKA DAR


JENERALI Umlimwengu akizungumza katika warsha ya wahariri kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika mchakato wa Katiba mpya, iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Profesa Issa Shivji.

BAADHI YA wahariri wakiwa katika warsha ya wahariri kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika mchakato wa Katiba mpya, iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Profesa Issa Shivji. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Mkubwa Ally na Mhariri Mtendaji wa Uhuru Publications Ltd, Josiah Mufungo.

TONITE IS EXTRAORDINARY FRIDAYS @ MILLENIUM LADIES FREEE B4 MIDNITE & FELLAS B 4 11PM..HAPPY HOUR 6PM-10PM COME EARLY SAVE MONEY!!


Kwa wale wadau wote wa DMV Mnakaribishwa tena leo Ijumaa ndani ya ukumbi wa Millennium Nite Club, mitaa ya kavurugeni muondoke, 1151 UNIVERSITY BLVED E, 20783. Parking zakumwaga Full misosi kama kawaida njooni mjione.

Kenyan woman in Wichita KS in critical condition after being attacked with a hammer

WICHITA, KS _A man who police say nearly killed a woman early this week by repeatedly striking her in the head with a hammer was charged Wednesday with attempted first-degree murder. Gideon K. Maiyo, 29, is accused of beating Elizabeth Kogo, 29, in an apartment in the 8100 block of East Harry on Sunday night. She was taken by ambulance to Wesley Medical Center, where she remained in critical condition Wednesday. 

Police said Maiyo left the apartment after the beating but was arrested after crashing his vehicle on the Kansas Turnpike. Police said Maiyo and Kogo are Kenyan nationals who have been in Wichita since 2008. Police said Maiyo is the defendant in a pending misdemeanor battery case stemming from an incident that occurred late last year. Kogo was the alleged victim in the case. 

Police said Kogo was cooperating with them in the battery case but asked that no restraining order be issued against Maiyo. District Judge Warren Wilbert set Maiyo’s bond at $100,000 and scheduled a Feb. 9 preliminary hearing. The Public Defender’s Office was appointed to represent him. Last year, close to 7 Kenyans including young children here in the USA lost their lives after severe domestic violence perpetrated by enraged husbands or boyfriends.

WATAMANI MIHOGO YA KUCHOMA ZANZIBAR…!!!


Baadhi ya Watalii kutoka nchi za Ulaya wakipata maelezo kutoka kwa mchuuzi wa mihogo ya kuchoma kuhusu chakula hicho wakati walipopita kwenye mtaa wa mchambawima mjini Zanzibar leo mchana wakiwa katika matembezi ya kujioneka sehemu mbalimbali za Kihistoria za Mjimkongwe. Picha na Matin Kabemba.

Mwizi wa Banki Ndani ya Mitaa Ya Kavurugeni Muondoke!


Mitaa ya tukio la uibaji wa benki ndania ya takoma park maryland.


Mtuhumiwa mmoja kwajina bado lipo katika uchunguzi aliojaribu kutaka kuiba benki ya Capital One ndani ya mitaa ya Takoma Park, Maryland na Prince George's County, na kuliwa hapo hapo katika tukio hilo mida ya 9:30 am asubuhi hii ya leo ijumaa jan,28/2011 Wandishi wa habari wa channel za kispanish leo walimiminika katika eneo hili marufu kwa langly park. katika tokeo la uibaji wa benki hiyo.