Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 Milaadiya, kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla,na kuwatakia amani na utulivu pia amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali yao kwa michango mbali mbali kuliletea maendeleo ya Taifa letu.
Picha na Ramadhan Othman IKULU. SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar katika mwaka 2012 itaendelea kuimarisha miundombinu na ubora wa huduma za jamii zikiwemo elimu, afya na maji safi na salama ili kwa pamojavisaidie kufikia lengo la kukuza uchumi na kupunguza umasikini, bila ya kuisahau dhamira
kuu ya Mapinduzi ya Kilimo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, katika risala aliyoitoa ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2012, AD na mwaka 1433 AH kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kwa jumla.
Katika risala yake hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa katika mwa 2012, Serikali itaongeza
ushirikiano na sekta binafsi katika kuchangia ukuaji wa uchumi na huduma za jamii.
Alieleza kuwa katika kukabiliana na athari za uchumi wa dunia hususan ongezeko la bei ya
chakula, Serikali imejidhatiti kukabiliana na tatizo hilo kwa kuimarisha sekta ya kilimo ili
kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima.
Akieleza mipango ya kiuchumi kwa mwaka 2012 Dk. Shein alisema kuwa Serikali inaazimia kuzidi kuongeza ukusanyaji wa kodi na kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
kuwa kila mmoja wetu anafaidika na sekta hii, huku tukiwa makini juu ya athari zake, na kwa
hivyo kuulinda utamaduni, mila na silka zetu´alisema Dk. Shein.
Alisema kuwa mazingira ya Utumishi bora katika kuwatumikia wananchi yatazidi kuimarishwa ili iwe chachu ya maendeleo ya haraka na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Alieleza kuwa masuala mengine yanayopaswa kukubushwa na kuyazingatia ni matukio makubwa ya Kitaifa likiwemo mchakato wa Katiba mpya ambapo ushiriki wa kila mmoja unahitajika na kuwanasihi wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni yao wakati utakapofika.
Aidha, alieleza jambo jengine la pili ni Sensa ya Taifa ya Watu na Makaazi, ambalo nalo ni tukio muhimu nchini kwani inapojulikana idadi ya watu ndipo upangaji bora wa huduma za
uchumi na jamii unavyofanyika kwa ufanisi.
Kutokana na umuhimu huo wa Sensa, alitoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano katika zoezi hilo
muhimu na kuwataka kuondoa hofu katika kujibu maswali watakayoulizwa na maafisa wa Sensa katika zoezi hilo litakalofanyika tarehe 26 Agosti, 2012.
Dk. Shein alisisitiza kuwa katika kuelekea mwaka 2012 kuna mambo muhimu ya kuyazingatia na kuyatekeleza ipasavyo kwa ustawi wa maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha amani na utulivu.
Jambo jengine ambalo Dk. Shein alilitaja ni kuongeza jitihada katika kukabiliana na vitendo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira na kushusha hadhi na haiba ya mji.
Kutokana na hali hiyo Dk. Shein aliwataka wananchi wote kushirikiana na viongozi, taasisi za serikali na zisizo za Kiserikali katika kuondoa taka, kuzuwia uchimbaji ovyo wa mchana, Soma zaidi othmanmapara.blogspot.com