Tuzungumze hili na Madaktari Mkuu.......Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(kushoto) akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na juu yao wanaonekana waziri wa fedha Mustafa Mkulo akiteta na Waziri wa UTUMISHI Hawa Ghasia ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali ya wabunge kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na uondoaji wa tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini na kufafanua kuwa serikali inaendelea na mikakati ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma ya umeme katika maeneo yasiyo na huduma hiyo na kuimarisha uzalishaji wa umeme wa uhakika katika Gridi ya Taifa kupitia vyanzo mbalimbali. Kwa picha zaidi tembelea Mrokim.Blog

No comments:
Post a Comment