Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Friday, February 24, 2012

IRAN KULETA MAKOCHA WA RIADHA NCHINI TANZANIA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia) akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na michezo ikiwemo kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha.

Balozi wa Irani nchini Tanzania (katikati) Movahhedi Ghomi akimweleza jambo waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam cha Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanueli Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Iran waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments:

Post a Comment