
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akiwa pamoja na Viongozi wengine wa kitaifa wa Serikali hiyo katika harakati za mazishi ya Mwakilishi wa Jimbo la Bububu CCM Marehemu Salum Amour Mtondoo yaliyofanyika huko kijijini kwao Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishiriki kumuombea dua aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu CCM Marehemu Salum Amour Mtondoo aliyefariki jana kutokana na ugonjwa wa shindikizo la damu huko katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa hotuba kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi CCM kuhusu utendaji kazi wa Marehemu katika chama hicho enzi za uhai wake

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein watatu kulia akiitikia dua iliyokuwa ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Skh. Omar Kaabil,kuliani kwa Rais ni Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi,kushotoni kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd

Wanawake mbali mbali waliojitokea katika mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu CCM Marehemu Salum Amour Mtondoo aliyefariki jana kutokana na ugonjwa wa shindikizo la damu huko katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
No comments:
Post a Comment