Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Sunday, April 8, 2012

ARSENAL WAISAFISHIA NJIA YA UBINGWA MAN UNITED

BAO la Mikel Arteta dakika za majeruhi usiku huu limetosha kuipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Emirates, London.

Arteta alifunga bao hilo dakika ya saba baada ya dakika 90 za kawaida za mchezo huo kutimia.
Sasa, matumaini ya Man City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu yanaelekea kuota mbawa, kwani imefikisha pengo la pointi nane dhidi ya vinara, Manchester United waliopo kileleni.

City ilimpoteza Yaya Toure aliyeumia mapema tu kwenye mchezo huo na bahati mbaya zaidi kwao mshambuliaji Mario Balotelli alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Alex Song.

Arsenal sasa imefikisha pointi 61, baada ya kucheza mechi 32- inazidiwa pointi 10 na Man City iliyo nafasi ya pili.

Mapema leo, mabao ya Wayne Rooney kwa penalti dakika ya 15 na Paul Scholes dakika ya 68, yaliipa timu hiyo ushindi wa 2-0 dhidi ya QPR na kuzidi kupaa kileleni.

Habari kwa hisani ya Mamapipiro.Blog

No comments:

Post a Comment