Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Friday, April 6, 2012

UCHAGUZI WA DMV UTAFANYIKA APRIL 15 SANDALY ANAOMBA KURA ZENU

Mh. Iddi Sandaly akiwa katika kiwanja cha Ager Road Hyattsville Maryland akifanya kampeni za uchaguzi wa DMV kwenye  kinyanganyiro cha uchaguzi utakao fanyika siku ya Jumapili April 15 wiki ijayo kwenye ukumbi wa  Mirage uliopo Hyattsville Maryland.

Katika kinyanganyiro cha uongozi wa juu wa jumuiya ya watanzania waishio hapa DMV, Ndugu Iddi Sandaly amekuwa Mmoja wa wagombea wa nafasi ya uongozi wa jumuiya hii.

Amekuwa shupavu ,mbunifu muaminifu, na mchapa kazi hodari kama tunavyomuelewa katika ushirikiano wake nasi vijana wa hapa DMV,

Hivyo amewaomba mumuunge mkono kwa kumpa kura zenu kwa wingi ili apate kuleta mabadiliko katika jumuiya.

No comments:

Post a Comment