If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, May 31, 2016

Kuongezeka mashambulizi ya utumiaji silaha nchini Msumbiji

Msemaji wa polisi ya Msumbijii amesisitiza kuwa, kushadidi mashambulizi ya utumiaji silaha nchini humo ni jambo linalotia wasiwasi.

Inacio Dina, msemaji wa polisi ya Msumbiji ameongeza kuwa watu wasiopungua 25 wameuliwa na kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wenye mfungamano na chama cha upinzani cha Renamo katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo. Ameongeza kuwa hali ya mambo ya Msumbiji hivi sasa ni ya kutia wasiwasi.

Siku kadhaa zilizopita wanamgambo wenye mfungamano na chama cha upinzani cha Renamo walipambana vikali na vikosi vya jeshi la Msumbiji katika jimbo moja magharibi mwa nchi na kusababisha vifo vya wanajeshi 45.

Chama cha upinzani cha Renamo ambacho kwa muda wa miaka 16 kilikuwa moja ya sababu kuu za kutokea vita vya ndani huko Msumbiji kutokana na kuungwa mkono na baadhi ya nchi ajinabi, kwa mara nyingine tena kimetoa vitisho kwa viongozi wa kisiasa wa Msumbiji kuwa kitaanzisha machafuko mapya nchini. 

Msumbiji imeendelea kubaki nyuma kiustawi kwa kukosa amani na uthabiti wa kisiasa na kiuchumi licha kupita miongo minne tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Chanzo: kiswahili.irib.ir

No comments:

Post a Comment

Maoni yako