If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, June 15, 2016

Aliyekuwa mgombea urais wa upinzani Kongo Brazzaville atiwa nguvuni

Chama cha upinzani cha l'IDC-FROCAD nchini Jamhuri ya Kongo kimetangaza kuwa aliyekuwa mgombea wake wa urais Jenerali mstaafu Jean-Marie Michel Mokoko ametiwa nguvuni na vyombo vya dola.

Michel Mokoko, mwenye umri wa miaka 69, ambaye aligombea urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu, alikuwa ndiye mpatanishi katika mchakato wa mgawanyo wa madaraka wakati wa vita vya ndani vilivyotokea nchini humo katika muongo wa 1990.

Ingawa serikali haijatoa tamko la kueleza sababu ya kumtia nguvuni Michel Mokoko ambaye aliwahi pia kuwa mshauri wa usalama wa Rais, lakini serikali hiyo ya Rais Denis Sassou Nguesso imemtuhumu jenerali huyo mstaafu kuhusika na jaribio la mapinduzi ya kijeshi la mwaka 2007.

Msemaji wa chama cha FROCAD Guy Romain Kinfouissia, amesema hatua hiyo inalenga kuzima nguvu ya upinzani na kutaka kumdhuru Jean-Marie Michel Mokoko ambaye alichuana na Rais Sassou Nguesso katika uchaguzi uliopita wa rais.


Ukiondoa kipindi cha miaka mitano tu, Sassou Nguesso ameitawala Jamhuri ya Kongo Brazaville kwa kipindi chote cha miaka 37 iliyopita. Alishinda tena katika uchaguzi uliolalamikiwa wa mwezi Machi ambao ulisusiwa na karibu vyama vyote vya upinzani, ingawa Michel Mokoko alishiriki na kushika nafasi ya tatu.

Mwaka uliopita Rais Sassou Nguesso aliitisha kura ya maoni ya kuifanyia mabadiliko katiba ili kumwezesha kugombea urais kwa muhula wa tatu kama walivyofanya viongozi wengine kadhaa wa nchi za Afrika. Uamuzi huo ulilalamikiwa na kuzusha machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 18 ambao waliuliwa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako