If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 10, 2016

IEBC: CORD YAKATAA IDADI KUBWA YA WANACHAMA WA JUBILEE

Na BERNARDINE MUTANU na LEONARD ONYANGO

MUUNGANO wa Cord umekataa orodha ndefu ya wanachama wa upande wa serikali walioteuliwa kushiriki meza mduara ya mazungumzo kumaliza Mrengo wa Jubilee umeteua kundi la wanachama 12 katika juhudi za kumaliza mzozo unaoshuhudiwa kuhusiana na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) kwa njia ya mazungumzo.

Kalonzo Musyoka
Kalonzo Musyoka pamoja na viongozi wengine wa muungano wa Cord wawahutubia wanahabari jijini Nairobi Juni 9, 2016. Picha/LEONARD ONYANGO

Viongozi wa upinzani wamechukua msimamo huo wakidai meza ya mdahalo itageuzwa kuwa 'soko la kelele' ikiwa itahusisha wanachama wengi.


"Kwa kweli meza ya kutatua mzozo kuhusu makamishna wa IEBC haifai kuwa na wanachama wengi," ikasema taarifa ya muungano wa CORD.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM Bw Philip Etale amethibitisha japo akasema kuwa vinara wa Cord wangetoa tangazo rasmi baadaye Alhamisi. 

Jubilee imechagua wanachama kumi na mmoja.

Wametajwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutimiza ahadi aliyotoa akiwa na Naibu wa Rais William Ruto mnano Jumatano.


Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ni mmoja kati ya wanachama hao watakaotarajiwa kushirikiana na wenzao kutoka upinzani Cord kumaliza mzozo huo.

Kundi hilo lilitangazwa Alhamisi baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Ruto kukutana na wabunge na maseneta wa Jubilee Ikulu Alhamisi.

Wanachama wa kundi hilo ni Maseneta Kiraitu Murungi (Meru), Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet), Beatrice Elachi (seneta maalumu), Fatuma Dullo (seneta maalumu), Wabunge Cecile Mbarire (Runyenjes), Naomi Shaban (Taveta), Moses Kuria (Gatundu Kusini), Jimmy Angweyi (Kitutu Chache Kaskazini).

Wengine walioteuliwa ni msaidizi wa kibinafsi wa Rais Kenyatta Jomo Gecaga, MP Ben Washiali (Mbunge) Mumias, Mohammed Mahmoud, na mwakilishi wa wanawake wa Narok Narok Bi Soipan Tuyak.

Wakati wa mkutano na wanahabari Jumatano, Rais Kenyatta akiandamana na Naibu Ruto alitangaza kuwa Jubilee ilikuwa imekubali mazungumzo kuhusiana na suala la IEBC.

Rais alisema hatua hiyo alichukua baada ya kukutana na Spika wa Bunge la Kitaifa na lile la Seneti pamoja na viongozi wa kidini.

Lakini Rais alisema mazungumzo hayo yangefanywa chini ya Katiba.

"Tunatarajia kuwa njia zingine kupitia Bunge zitatumiwa ndani ya kamati ya pamoja,” alisema Rais Uhuru Kenyatta.

Wanakamati wa Cord

Awali, Cord ilikuwa imeteua wawakilishi wake ambao walitarajiwa kuwakilisha mrengo huo katika mazungumzo na wenzao wa Jubilee kumaliza mzozo wa IEBC lakini nje ya Bunge.

Walikuwa ni pamoja na Seneta Johnstone Muthama wa Machakos, Seneta James Orengo (Siaya), Eseli Simiyu (Mbunge wa Tongaren) Mwakilishi wa Wanawake wa Mombasa Mishi Mboko na Junet Mohammeds, Mbunge wa Suna Mashariki.

Wakati huo huo, viongozi wa Cord wakiongozwa na Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetang’ula walikuwa na msururu wa mikutano ambapo walikutana na viongozi wa makanisa na Balozi wa Amerika humu nchini Robert Godec.

Akihutubia wanahabari baada ya kukutana na viongozi wa kidini Bw Kalonzo alisema kwamba mazungumzo yao yalielekea kutatua utata unaogubika IEBC.

“Tunaendelea kujadiliana na kuna matumaini kwamba huenda tukapata suluhisho,” akasema Bw Kalonzo.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa nchini (NCCK) Canon Peter Karanja amewataka Wakenya kuombea utata kuhusu IEBC huku akisema kwamba viongozi wa dini wamepiga hatua kubwa katika kutatua mvutano uliopo kuhusu makamisha wa tume hiyo.

“Msuala yanayozua utata baina ya Cord na Jubilee yanaelekea kupungua na huenda tukapata suluhisho hivi karibuni,” akasema Kasisi Karanja.

Sasa yamkini Cord itachukua hatua ya kushinikiza Jubilee kupunguza idadi ya wawakilishi wake watakaoshiriki mazungumzo kuhusu IEBC.

“Ikiwa kila upande utatoa wawakilishi 11, inamaanisha kwamba kutakuwa na watu 22 watakaoshiriki mazungumzo hayo. Idadi hiyo ni kubwa na huenda wakakosa kuafikiana. Ni vyema kila upande uwakilishwe na watu watano pekee,” akasema mbunge aliyetaka jina lake libanwe kwa kuwa hana ruhusa ya kuzungumza kwa niaba ya Cord.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako