If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, June 1, 2016

KENYA: UAMUZI KUWAREJESHA WAKIMBIZI KWAO ULIKUWA WA MWISHO!

Na BERNARDINE MUTANU

SERIKALI imesisitiza kuwa uamuzi wa kuwarejesha wakimbizi makwao ulikuwa wa mwisho.

Joseph Nkaissery
Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery ahutubia wanahabari akiwa pamoja na viongozi wengine serikalini Mei 31, 2016 jijini Nairobi. Picha/BERNARDINE MUTANU

Katika mkutano na wanahabari wakati wa kupokea ripoti kutoka kwa jopo maalum kuhusiana na jinsi ya kuwarejesha wakimbizi kwa kuzingatia ubinadamu, Waziri wa Masuala ya Ndani Joseph Nkaissery alisema serikali haitarudi nyuma kuhusiana na uamuzi wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Daadab.

“Uamuzi wa kufunga kambi ni wa mwisho. Shughuli ya kuwarudisha wakimbizi itaanza hivi karibuni. 

Tutawasilisha ripoti kwa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi,” alisema Bw Nkaissery.

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto tayari wametoa kauli kuhusiana na suala hilo kwa kusisitiza kuwa wakimbizi watarejeshwa makwao kutokana na tishio la kiusalama na kiuchumi nchini.

Serikali iliahidi kutoa Sh1 bilioni kufanikisha zoezi hilo.


“Lazima watarejeshwa makwao na mataifa mengine yaliyo tayari kuwachukua. Ifikiapo Novemba 2016, shughuli hiyo inafaa kuwa imekamilika,” alisema Waziri Nkaissery.

Kulingana na makubaliano kati ya Kenya, Somalia na UNCHR, wakimbizi walifaa kujirejesha makwao kwa kupenda.

Shughuli kujikokota

Lakini serikali ya Kenya inahisi kwamba shughuli hiyo inaenda polepole sana huku taifa likizidi kutishiwa na magaidi.

Mei 31, 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya jopo hilo kuwasilisha ripoti kuhusiana na jinsi inayofaa katika zoezi la kufunga Daadab.

Jopo hilo likiongozwa na Bw Joseph Irungu na Dkt Gordon Kihalangwa lilifaa kubuni mikakati ya kuwarejesha wakimbizi Somalia, kipindi cha kukamilisha zoezi hilo na gharama ya zoezi hilo.

Mwenyekiti, Bw Irungu alisema walikuwa wametilia maanani matakwa yote saba kutoka kwa serikali na kuhusisha wadau wote katika kubuni ripoti hiyo.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako