If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 13, 2016

KENYA: WASIOMTAMBUA MUNGU WAAPA KUISHTAKI SERIKALI KWA KUBAGULIWA

MUUNGANO wa Wakenya wasiomcha Mungu (AIK) umesema utaenda mahakamani kuishinikiza Serikali ibatilishe uamuzi wa kuupiga marufuku.

Harrison Mumia
Bw Harrison Mumia, 35, anayefanya kazi Benki Kuu ya Kenya ambaye haamini kwamba Mungu yupo. Picha/GERALD ANDERSON

Kiongozi wa muungano huo, Bw Harrison Mumia Jumapili alithibitisha kupokea barua iliyofutilia mbali usajili wa muungano huo kutoka kwa afisi ya Mwanasheria Mkuu, lakini akalalamika ilitumwa kwao kuchelewa.

Kulingana na Bw Mumia, barua hiyo iliyoandikwa na Naibu Msajili wa mashirika Bi Muluku Kariuki, ilipokelewa Juni 10 ilhali ilikuwa imeandikwa Aprili 29.

“Mbona haikutumwa kwetu kwa barua pepe? Mbona msajili hakutuita kuichukua kutoka kwa afisi yake? Tuna maswali mengi,” akasema kwenye taarifa kwa waandishi wa habari.


Barua hiyo ya Bi Kariuki ilikuwa imesema usajili wa muungano huo utakuwa umefutiliwa mbali siku saba kuanzia siku ambapo barua iliandikwa.

Sababu zilizotolewa ni kuwa afisi ya Mwanasheria Mkuu inayosimamiwa na Prof Githu Muigai ilikuwa imepokea malalamishi mengi kuhusu matamshi ya muungano huo, ambayo yanaweza kutatiza amani nchini.

Lakini Bw Mumia alilalamika kuwa uamuzi huo unakiuka haki za wanachama wake kwa kuwa Kenya si taifa linalotawaliwa kwa misingi ya sheria za kidini.

“Serikali haifai kushinikizwa na kundi lolote la kidini kufanya maamuzi hasa kuhusu mambo muhimu ya uhuru wa kuabudu wa Wakenya wote,” akasema.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako