If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 10, 2016

MBUNGE ADAI RAILA ATATENGWA NA VINARA WENZA 2017

Na MWANGI MUIRURI

MBUNGE wa Gichugu Bw Njogu Barua sasa anamuonya kinara wa Cord Bw Raila Odinga kuwa huenda abakie ametengwa na vinara wenza wake uchaguzi mkuu wa 2017 ukikaribia.

Raila Odinga
Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga akihutubu awali. Picha/KEVIN ODIT

Alidai kuwa “mimi najua kuhusu njama kali ya kuwavuta vinara wenza wa Bw Raila ambao ni Bw Kalonzo Musyoka na Seneta wa Bungoma Bw Moses Wetang'ula hadi Jubilee.”

Alisema kuwa njama hiyo ni mojawapo ya zingine nyingi ambazo zimeimarishwa kichinichini za kumwezesha rais Uhuru Kenyatta na serikali yake anachaguliwe kwa awamu ya pili katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Akiongea katika eneo la Kianyaga Alhamisi, Bw Barua alisema kuwa “lengo kuu la serikali ni kuibuka na ushindi kwa asilimia 60 katika uchaguzi huo.”

Akasema: “Wacha nitoe tahadhari kwa kinara wa Cord Bw Raila kuwa wakati serikali itangurumisha uwezo wake wa kuchapa kampeni, atashtukia amehamwa na vinara wenza wake wote. Atabakia tu kuwa mwanasiasa asiye na udhabiti wa kupambana.”


Matamshi hayo ya Bw Barua yaliwiana na ya mbunge wa Gatundu Kusini Bw Moses Kuria ambaye Jumatano akiongea katika eneo la Gatundu alisema kuwa serikali inajadiliana na Bw Kalonzo na Bw Wetang'ula kuhusu kujiunga pamoja na serikali.

Licha ya kuwa Bw Wetang'ula mara kadhaa amejitokeza hadharani kusema kuwa yeye yuko ndani ya Cord na hatang’atuka kwa kuwa alikuwa mwanzilishi wa muungano huo, Bw Kuria alisema kuwa “wakati wowote utashuhudia Bw Kalonzo na Bw Wetang'ula wakijumuika ndani ya serikali.”

Kupeperusha bendera ya Cord

Pia, Bw Kalonzo amekuwa ngangari kuwa atakaa ndani ya Cord akitumainia kuwa atapewa majukumu ya kupeperusha bendera kama mgombezi wake wa urais katika uchaguzi wa 2017.
Bw Kuria alisema kuwa “tayari tumekuwa tukishauriana na wandani wa wawili hao na kufikia sasa tumepiga hatua muhimu mbele katika kuafikiana jinsi ya wawili hao watatuunga mkono na kwa manufaa gani.”

Bw Barua alisema kuwa “ukiangalia namna maeneo ya Ukambani na Magharibi yamekuwa yakicheza siasa zao katika siku za hivi majuzi, utakubaliana nami kuwa najua kuhusu ninayokuambia sasa kuhusu mtandao wa serikali kuvutia maeneo hayo.”

Alisema kuwa uchaguzi mdogo wa Malindi wa 2015 “ndio uliandaa mikakati yetu ya kujaribu kunyakua maeneo yanayokisiwa kuwa ngome ya Bw Raila na lengo letu kuu ni kupunguza ufuasi wake katika maeneo hayo kwa asilimia 20.”

Akasema: “Tayari tuko na ratiba ya kufanya hivyo na kwa sasa utekelezaji umeandaliwa. Ukifuatilia ziara za rais Uhuru Kenyatta za kikazi katika maeneo tofauti ya hapa nchini utashuhudia kuwa tumejipanga. Tuseme tu kwa wakati huu hatujaingia katika msimu wa siasa kamili ili tuzindue mtandao wetu wa kampeni.”

Alisema hayo huku rais akianza ziara yake ya siku nne katika maeneo ya Ukambani ambapo kinachobishaniwa ni kura zaidi ya 1.2 milioni za jamii hiyo na ambapo kumejitokeza mirengo miwili inayoonekana kutoshana nguvu ya ufuasi wa Cord na Jubilee.

Kati ya wabunge 22 ambao wamechaguliwa katika eneo hilo, 11 wanaonekana kuegemea katika mrengo wa Gavana wa Machakos Bw Alfred Mutua na ambaye huashiriwa kuwa na uchumba na serikali ya Jubilee huku 11 wakiegemea mrengo wa Bw Kalonzo ndani ya Cord.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako