If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 2, 2016

Mfalme wa Saudia akumbwa na matatizo ya kiakili, haruhusiwi kuona wageni

Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia amekumbwa na maradhi mabaya mno ya kiakili kiasi kwamba wageni wanazuiwa kumtembelea. Mwanae Mfalme Salman ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Naibu Mrithi Kiti cha Ufalme, Mohammad bin Salman ametoa amri ya kupiga marufuku wageni kumtembelea baba yake ambaye ana maradhi sugu ya kiakili.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Kipalestina la Manar toleo la Jumatano, duru mjini Riyadh zinadokeza kuwa, wageni kutoka nchi za nje na hata watu wa ukoo wa kifalme wa Aal Saud hawaruhusiwi kumuona Mfalme Salman.

Imearifiwa kuwa, balozi za kigeni, hasa ubalozi wa Marekani mjini Riyadh, unafuatilia kwa karibu hali ya Kiafya ya Salman kwani kuna wasiwasi mkubwa kuwa yamkini mgogoro mkubwa ukaibuka endapo mfalme huyo ataaga dunia.

Mfalme Salman mwenye umri wa miaka 80 anaaminika kuugua ugonjwa wa kupoteza fahamu wa Alzheimer na kwamba ufalme wa Saudia kimsingi unaendeshwa na Mohammad bin Salman. 

Mashahidi wanasema mfalme huyo wa Saudia huwa anapoteza fahamu mara kwa mara na anaweza kusahau alichokisema dakika chache zilizopita au watu ambao amewajua umri wake wote.


Aidha duru za karibu na ufalme wa Saudia zinadokeza kuwa, mfalme huyo amepata matibabu hospitalini mara kadhaa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Kutokana na hali hiyo mbaya ya mfalme Salman, imedokezwa kuwa vita vya kuwania uritihi wa kiti hicho vimepamba moto ndani ya ukoo wa Aal Saud. Inasemekana Mfalme Salman amekuwa na mpango wa kumweka kando mrithi wa kwanza wa kiti hicho, Muhammad bin Nayef na badala yake kumrithisha mwanawe kiti hicho.

1 comment:

  1. Muandishi hakikisha habari kabla ya kuchapisha ,Saudi king yuko mzima na juzi 31 may walikuwa na mkutano wao wa GCC , ulofanyika Jiddah na yeye yumo hata kwenye news tizama na mkutano ulikuwa live unsoneshwa TV zote za Kiarabu

    ReplyDelete

Maoni yako