If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, June 12, 2016

MUTUNGA SASA ATETEA MAANDAMANO YA CORD

Na VALENTINE OBARA

JAJI Mkuu Willy Mutunga ametetea maandamano ya Muungano wa Cord na kutaka polisi wabadilishe mbinu zao za kutoa usalama wakati wa maandamano.

 Willy Mutunga
Dkt Willy Mutunga. Picha/MAKTABA

Jaji Mkuu Willy Mutunga ametetea maandamano ya Muungano wa Cord na kutaka polisi wabadilishe mbinu zao za kutoa usalama wakati wa maandamano.

Dkt Mutunga amesema maandamano ni haki ya kikatiba kwa wananchi na ni jukumu la polisi kulinda waandamanaji pamoja na wananchi wengine.

“Polisi ndio wenye jukumu la kuhakikisha wanakamata na kushtaki wezi na watu wanaozua vurugu wakati wa maandamano. Inawezekana hata wanaobeba mawe huwa si waandamanaji,” akasema.

Alikuwa akizungumza katika Kanisa Katoliki la St John’s lililo mtaa wa Korogocho, Kaunti ya Nairobi alipohojiwa na mwanahabari James Smart.


Dkt Mutunga ambaye amepanga kustaafu wiki hii aliongeza kuwa Inspekta Jenerali Joseph Boinnet anafaa awe akizungumza na waandalizi wa maandamano yoyote ili waone jinsi ya kudumisha utulivu wakati wa maandamano badala ya kuyapiga marufuku, kwani hiyo ni kinyume cha katiba.

Bw Boinnet aitoa taarifa Jumapili kutaka viongozi wa Cord waarifu polisi kuhusu wakati watakapoanza na kukamilisha maandamano yao Jumatatu na Alhamisi, idadi ya waandamanaji wanaotarajiwa na barabara wanazopanga kutumia ili polisi wajiandae kutoa usalama.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako