If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, June 15, 2016

Polisi Kenya wawasaili wanasiasa wanatoa matamshi ya chuki

Polisi nchini Kenya wamewasailia wanasiasa saba wapinzani na wanaounga mkono serikali kwa kosa la kutoa matamshi ya chuki huku uhasama wa kisiasa ukishika kasi nchini humo mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Wanasiasa hao saba ambao ni wabunge na seneta ni pamoja na Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na Ferdinand Waititu kutoka upande wa serikali na Junet Mohammed, Aisha Jumwa, Johnson Muthama na Timothy Bosire kutoka muungano wa upinzani wa CORD unaoongozwa na Raila Odinga.

Inasemekana kuwa Kuria, alitoa tamko dhidi ya Raila lakini amekana kutoa matamshi hayo.

Wabunge wa upinzani nao wanadaiwa kutoa matamshi ya kuwachochea wafuasi wao dhidi ya muungano unaotawala wa Jubilee. Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Kenya (DCI), Ndegwa Muhoro, amesisitiza suala la kufuata mkondo wa sheria kwa kusema washukiwa wa matamshi ya chuki watafikishwa mahakamani.

Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wakiwa wamekamatwa na wengine kujiwasilisha katika Idara ya Ujasusi wa Jinai (DCI) kuandikisha taarifa kwa kudaiwa kutoa matamshi ya chuki.

Wakati huo huo Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa inayoongozwa na Mwenyekiti Francis Ole Kaparo sasa inawazia kuunda mahakama maalumu ya kushughulikia kesi zinazohusu matamshi ya chuki.

Haya yamesemwa na Ole Kaparo kwenye kikao na wanahabari akihutubia taifa kuhusu hali ilivyo nchini ikizingatiwa kuwa baadhi ya wanasiasa wa Jubilee na CORD wanakabiliwa na tuhuma za kutoa matamshi ama dhidi ya kabila fulani au kuchochea na kuzua uhasama kwa ujumla nchini Kenya.

Katika wiki za hivi karibuni muungano wa CORD umekuwa ukiitisha maandamano kila Jumatatu kote nchini Kenya kushinikiza Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) iondoke kwa madai kuwa inapendelea upande wa serikali. Hata hivyo Rais Uhuru Kenyatta anasisitiza kuwa tume hiyo inapaswa kuondolewa kwa kufuata mkondo wa sheria bungeni na wala si maandamano ya mitaani.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako