If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 4, 2016

Tanzania: Wakaazi wa kijiji kulikojiri mauaji Tanga wahama

Wakaazi wa kijiji cha Kibatini mkoani Tanga huko Tanzania wamekihama kijiji chao kufuatia mauaji ya kutisha yaliyotokea katika eneo hilo.

Duru zinaarifu kuwa, wasiwasi umetanda katika kijiji hicho baada ya watu wanane kutoka kijiji cha Kibatini kwenye kata ya Amboni kuchinjwa kama wanyama na watu wasiojulikana Jumatatu usiku. 

Taarifa zinasema kuwa, wanakijiji 70 wameshaondoka katika kijiji cha Kibatini, Wadi ya Mzizima na kuhamia kijiji cha Corner Z katika wadi hiyo. 

Wanakijiji hao wamehama makazi yao kwa kuhofia maisha yao hata baada ya polisi kuwahakikishia usalama wao. Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruk (CUF), amelazimika kukatisha vikao vya Bunge vinavyoendelea Dodoma na kwenda kuwahamisha wananchi wa Kibatini baada ya kutokea mauji ya watu wanane. 

Mbunge huyo amesema anaungana na wapiga kura wake akisema kwa sasa eneo hilo si salama kwa maisha. 

Sheikh wa Mkoa wa Tanga, Ali Juma Luuchu, aliiomba Serikali kushirikisha viongozi wa dini na wazee kutafuta suluhu ya kudumu ya matukio hayo yanaonekana kutamalaki katika jiji hilo. 


Alisema tukio hilo haliwezi kuachiwa serikali pekee kwa vile ni lazima wao kama viongozi wa dini washirikiane na kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa kwa sababu vinachafua sura ya mkoa wa Tanga na nchi kwa ujumla. 

Katika wiki za hivi karibuni watu kadhaa wameuawa kinyama kwenye maeneo mbalimbali Tanzania huku wananchi wakiingiwa na hofu na kuitaka serikali ichunguze sababu ya kuzorota usalama. 

Serikali ya Tanzania imesema kutuma kikosi maalumu cha ulinzi, kikiongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaka watu wanaoaminika kufanya mauaji hayo mkoani Tanga.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako