If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, June 14, 2016

UNHCR: Muda zaidi unahitajika kuwahamisha wakimbizi Wasomali nchini Kenya

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi, amesema serikali ya Kenya inapaswa kulegeza msimamo wake kuhusu muda wa mwisho iliotoa kwa ajili ya kuwarejesha makwao wakimbizi wapatao 350,000 Wasomali walioko nchini humo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi Grandi ametaka kurefushwa muhula huo wa mwisho wa mwezi Novemba uliotolewa na serikali ya Kenya akisisitiza kwamba hali si ya usalama hata kidogo katika baadhi ya maeneo ya Somalia wanakotaka kurejeshwa wakimbizi hao.

Mkuu wa UNHCR aidha ametoa wito kwa wafadhili kutoa msaada wa fedha kwa ajili ya kuandaa ajira na kuijenga miundombinu ya Somalia ili kuwawezesha wakimbizi Wasomali walioko kwenye kambi ya Dadaab, ambao wanataka kurudi makwao katika maeneo tisa ambayo kwa mujibu wa UN yana usalama, waweze kufanya hivyo.

Amesema hawataki kuwasaidia wakimbizi hao kurudi makwao kisha wakawe wakimbizi wa ndani huko Somalia.

Grandi amesema atakutana na viongozi wa serikali za Kenya na Somalia baadaye mwezi huu baada ya kuwashawishi wafadhili kuchukua hatua zaidi za uwekezeaji nchini Somalia ili kuboresha hali ya nchi hiyo.


Kenya ilitangaza mwezi uliopita wa Mei kuwa inapanga kuifunga kambi ya Dadaab iliyoko mashariki mwa nchi hiyo kwa sababu kambi hiyo kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ni chaka linalotumiwa na kundi la kigaidi la Al-Shabab la Somalia kujipenyeza na kuandaa magaidi wanaofanya mashambulio ya kigaidi ndani ya ardhi ya Kenya.

Kwa mujibu wa Mkuu wa UNHCR tangu Desemba 2014 hadi sasa ni wakimbizi 14,000 tu Wasomali walioamua kurudi makwao kwa hiyari yao huku wengine 8,000 wakiwa kwenye orodha ya wanaosubiri kufanya hivyo.../

No comments:

Post a Comment

Maoni yako