If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 11, 2016

Wabunge waja juu kiinua mgongo chao

WABUNGE wamechachamalia hatua ya Serikali kutaka kiinua mgongo chao wanachopaswa kulipwa baada ya miaka mitano ya kazi yao ya ubunge kitozwe kodi na kusema kuwa uamuzi huo si sahihi kwa kuwa utaminya maslahi yao na kulenga kuwasukuma kuwa ombaomba baada ya kustaafu kazi hiyo.

Naibu Spika Dk Tulia Ackson.
Naibu Spika Dk Tulia Ackson.

Aidha, imependekezwa kuwa, iwapo hakuna marekebisho yatakayofanywa na Serikali kuhusu kodi hiyo, tozo hilo la kodi liwahusu pia viongozi wote wa kisiasa, ili kuleta usawa katika maslahi.

Kama jinsi Kamati ya Bunge ya Bajeti ilivyowasilisha taarifa yake Bungeni kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2015/16, pamoja na tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2016/17, wabunge hao wa Kambi ya Upinzani kupitia taarifa yao na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walisema hatua hiyo haikuwa na umuhimu wowote kutajwa kipindi hiki, kwa sababu utekelezaji wake, ikiwa utapitishwa ni mwaka 2020.

Akitoa maoni ya Kamati hiyo ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Ghasia ambaye ni Mbunge wa Mtwara Vijijini, alisema kwa miaka mingi Bunge limekuwa mstari wa mbele kujadili na kupendekeza watumishi wa umma kusamehewa kodi kwenye malipo ya viinua mgongo wanavyolipwa.

“Bunge limekuwa likishauri hivi ukizingatia kuwa mishahara ya watumishi wa umma na hata viongozi wa siasa imekuwa ikikatwa kodi, hivyo hatua hii inayopendekezwa na Serikali inakuwa ‘double taxation’ (ikimaanisha kutozwa kodi mara mbili),” alisema.


Alisema ni muhimu Serikali ikafikiria suala hilo upya kurekebisha kodi hiyo na kama iishindikana ijumuishe viongozi wote wa kisiasa na si wabunge pekee. Wabunge mmoja mmoja wakichangia hoja akiwemo Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), aliyeeleza kuwa, hatua hiyo ya Serikali haiwatakii mema kwa sababu imelenga kukipunguza hata kile kiasi kidogo wanachojidundulizia kwa miaka mingi ili kiwasaidie wakati wakiwa wamestaafu ubunge.

Kwa maelezo yake, fedha wanazopata ambazo Serikali inaziona kuwa nyingi, huishia kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo, mara nyingi wabunge huombwa kuchangia michango ya wananchi wanaopatwa matatizo majimboni.

“Mheshimiwa Waziri wa Fedha anapaswa kufahamu kuwa sisi wabunge mshahara wetu ni mdogo sana kuliko wake na hatuna pensheni. Anapaswa kutambua kuwa, kule mitaani wabunge wamegeuzwa ATM kwa kuombwa fedha karibu na kila mtu, hivyo kuhitaji kuachiwa kiinua mgongo chetu kama kilivyo,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa wabunge ndio wanaopigania kila wakati mafao ya watumishi wengine wa umma yasikatwe kodi, hivyo Serikali iliangalie tena suala hili na kulifanyia marekebisho. Naye Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM), alisema, Ofisi ya Mbunge ni taasisi inayojitegemea na kwamba fedha zinazoonekana nyingi si za mbunge, bali ni za jamii, hivyo kukata kodi katika kiinua mgongo cha mbunge ni kumuumiza.

Kwa upande wa kambi ya Upinzani Bungeni, aliyewasilisha taarifa kwa niaba ya Msemaji Mkuu ambaye ni Waziri Kivuli wa Fedha na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde alisema, Serikali haijawataja Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya katika kundi la wanaopaswa kutozwa kodi ya kiinua mgongo, badala yake imewabana wabunge pekee.

Alisema, “tuko tayari kutoa ushirikiano kwa serikali kupanua wigo wa mapato kwa njia hiyo iwapo itawajumuisha viongozi hao iliowaacha.” Wakati huo huo, wabunge hao wameshawishiana kutokubali kutumika kama muhuri kwa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali, ikiwa itakuwa umeandaliwa na kuwasilishwa bungeni bila kujumuisha ushauri wa Kamati ya Bajeti, kama ilivyofanyika kwa ya mwaka wa fedha 2016/17.

Kuhusu suala hilo, Kamati ya Bajeti ilisema, kimsingi Serikali kutokuwa tayari kupokea ushauri wa kamati hiyo kuhusu bajeti si sahihi kwa sababu, wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanahitaji kujua namna Serikali itakavyotekeleza mahitaji ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao zinazowasilishwa na wabunge kupitia Kamati zao za kisekta.

Akishawishi wabunge wengine kukataa kutumika kama muhuri, Mbunge wa Mkinga (CCM), Dastan Kitandula alisema, “Wabunge tusikubali kuwa rubber stamp (muhuri wa kuidhinisha bajeti ya serikali), ikiwa ushauri wa Kamati ya Bajeti utakuwa umepuuzwa,” autapuuzwa.”

No comments:

Post a Comment

Maoni yako