If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 10, 2016

Wapinzani wa Nigeria wakataa kufanya mazungumzo na serikali

Kundi la waasi wa Nigeria linalojulikana kwa jina la 'Walipizaji Kisasi wa Niger Delta' Kwa mara nyingine tena limekataa pendekezo la serikali kuu ya nchi hiyo la kufanya mazungumzo ya kumaliza machafuko yanayoendelea kusini mwa nchi.

Kundi hilo limetangaza kuhusika na shambulio lililotekelezwa hivi karibuni kwenye jukwaa la mafuta la shirika la Marekani la Chevron. Kudhihiri kwa kundi hilo jipya la waasi bila shaka kunavuruga zaidi hali ya usalama wa kusini mwa Nigeria. 

Waasi hao wanataka kupewa hisa zaidi ya pato la mafuta yanayochimbwa huko Niger Delta, jambo ambalo Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo alitangaza wazi kulipinga katika kampeni zake za uchaguzi mkuu uliopita na kuahidi kuyamaliza kabisa makundi yote ya waasi yanayovuruga shughuli za uchimbaji mafuta na kuhatarisha usalama wa vituo vya mafuta katika eneo hilo. 

Hata hivyo serikali ya Abuja imelegeza msimamo wake kuhusu suala hilo ambapo ilitangaza hivi karibuni kwamba iko tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo na waasi wa Niger Delta kwa lengo la kutafuta njia za kumaliza ghasia na machafuko katika eneo hilo. 


Kuhusu kadhia hiyo Emmanuel Ibe Kachikwu, waziri mashauri anayeshughulikia masuala ya vyanzo vya mafuta katika serikaliya Nigeria, amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika mazunguzo kati ya serikali na waasi wa Niger Delta huku akisema kwamba vitendo vya waasi hao vimepunguza kwa kiwango kikubwa uzalishaji na mauzo ya mafuta ya nchi hiyo. 

Amesema machafuko ya waasi na kutokarabatiwa kwa taasisi za mafuta za eneo hilo ni mambo mawili makuu ambayo yamepunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji mafuta wa eneo hilo. Hivi sasa kudhihiri kwa kundi hilo jipya la waasi kumebadilika na kuwa jinamizi kwa serikali ya Nigeria. 

Mbali na kundi la Walipizaji Kisasi wa Niger Delta, makundi mengine ya waasi ya Harakati ya Serikali ya Utawala wa Ndani ya Biafra na Harakati ya Ukombozi wa Niger Delta yamevuruga sana usalama wa eneo hilo. 

Katika siku za hivi karibuni maandamano yaliyoitishwa na Harakati ya Serikali ya Utawala wa Ndani ya Biafra katika eneo hilo yaligeuka na kuwa vurugu kubwa kati ya waandamanaji na askari polisi ambapo watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. 

Eneo la Biafra katika nusu ya pili ya muongo wa 60 lilishuhudia vita vikubwa vya umwagaji damu ambavyo vilidumu kwa muda wa miaka miwili na miezi minane na kupelekea watu karibu milioni moja kupoteza maisha. 

Kugunduliwa mafuta katika eneo hilo na uchochezi uliofanywa na mashirika ya kigeni ya uchimbaji mafuta kwa uungaji mkono wa serikali za nchi yalikotoka mashirika hayo, ni sababu kuu iliyozua vita hivyo.

Licha ya kuwa miaka mingi imepita tokea kumalizika kwa vita hivyo kufuatia ukandamizaji wa kijeshi na kiuchumi wa serikali dhidi eneo hilo, lakini inaonekana kwamba hadi sasa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wangali wana hisia za kutaka kulitenga na Nigeria. 

Mgogoro wa kusini mwa Nigeria umeongezeka katika hali ambayo serikali ya nchi hiyo inakabiliwa na changamoto zingine kubwa na zinazopaswa kushughulikiwa kwa haraka zikiwemo za kiuchumi ambazo zinatokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa, mashambulio ya magaidi wa Boko Haram katika eneo la kaskazini, ulanguzi wa madawa ya kulevya na mashambulio ya maharamia katika maji ya Ghuba ya Guinea, mapigano ya kikabila katika jimbo la Borno na pia uingiliaji wa madola ya kigeni.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako