If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, November 8, 2016

KENYA: ATWOLI ASEMA WANAOMTUSI RAIS WAKOME KUMHUSISHA

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Bw Francis Atwoli, amewataka wakosoaji wa Rais Uhuru Kenyatta wamshambulie moja kwa moja bila ya kumhusisha yeye.

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli.
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli. Picha/MAKTABA

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa COTU, Bw Atwoli amejitenga na kauli za kumkashifu Rais Kenyatta zinazoaminika kutoka kwake na kuenezwa kupitia ukurasa wa Facebook unaoitwa ‘Kenya Political Forum’.

“Wakenya hizi ni propaganda tupu. Mwenye uhasama na rais amshambulie mwenyewe moja kwa moja, Francis Atwoli hasemi kupitia mawakala au maajenti,” Bw Atwoli alinukuliwa.

Bw Atwoli aliwaonya wakosoaji wa rais dhidi ya kutumia akaunti ghushi mitandaoni ili kumshambulia rais wakitumia jina lake.
Kauli iliyozua mtafaruku zaidi iliyochapishwa kwenye ukurasa huo wa Facebook na kumnukuu Bw Atwoli ni:

“Hatuwezi kuhatarisha kwa kumpa Uhuru Kenyatta miaka mingine mitano. Nyongeza hiyo itazidi kuijeruhi nchi hii na kuifanya kavu. Tutajidhulumu sisi, kizazi kijacho na kwa Mungu pia. Kenya ni kubwa kumshinda Uhuru mara milioni –Atwoli”.
Akana


Hata hivyo, Bw Atwoli ameikana kauli hiyo na nyinginezo zilizosambazwa kwenye mitandao ya Facebook, Twitter na WhatsApp.

Haya yanajiri baada ya bloga Alan Wadi mwaka jana kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kutozwa faini ya takriban Sh 200,000 baada ya kumtukana rais kupitia Facebook.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako