If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, November 10, 2016

KENYA: SITA WAFARIKI BAADA YA JENGO LA GHOROFA 10 KUPOROMOKA KISII

Na JADSON GICHANA na NYABOGA KIAGE

WATU sita walifariki na wengine 43 wakajeruhiwa Alhamisi asubuhi, jumba la ghorofa kumi lilipoporomoka mjini Kisii.

Ghorofa yaporomoka Kisii
Waokoaji wakishughulika baada ya ghorofa kuporomoka mjini Kisii Novemba 10, 2016. Watu sita walifariki na wengine kadhaa wakajeruhiwa. Picha/BENSON MOMANYI

Jengo hilo lilikuwa likijengwa katika eneo la Daraja moja mkabala na hospitali ya RAM mita chache tu kutoka kwa ofisi ya gavana James Ongwae.

Jengo moja ambamo watu wanaishi kando ya jengo lililoanguka pia liliathiriwa.

Tukienda mitamboni, watu 26 walikuwa wamelazwa hospitalini, baada ya wengine 17 kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

Iliwalazimu askari kuingilia kati na kuwatawanya watu ambao walikuwa wamezunguka eneo la mkasa.

Katika ghorofa ya chini kulikuwa na duka ambalo lilikuwa limefunguliwa na haikujulikana iwapo muuzaji wa duka hilo aliyesemekana kuwa mtoto alinusurika au la.

Kulingana na mkazi mmoja Bi Irene Akinyi ambaye alikuwa ameenda dukani kununua soda, alisikia mlio mkubwa na alipotizama juu aliona jumba likiporomoka.

“Ilinibidi nikimbilie maisha yangu nilipoona jengo likiporomoka. Wenzangu wamekwama ndani,” alisema Bi Akinyi.


Wengi wa wajenzi waliokuwa wakiendelea na kazi zao katika jengo hilo walinusurika kifo na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kisii na ile ya RAM.

Watoto saba waliokuwa katika ghorofa jirani pia walipata majeraha madogo na kukimbizwa katika hospitali ya Kisii.

Kulingana na Bi Eunice Kemunto ambaye ni mama wa watoto watatu kati ya walioumia, alikuwa ameenda kusukwa nywele aliposikia kisa hicho.

Ameambia Swahilihub kuwa alikuwa mwenye furaha kwani watoto wake waliponea kifo na hawakuwa wameumia sana.

“Siyaamini macho yangu. Watoto wangu wako sawa, hasara tu ambayo tumepata ni jumba hilo kuporomoka na kuathiri nyumba yangu,” alisema Bi ambaye ni mke wa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Manga.

Majeraha ya mgongo

Bw Robert Oreni, aliyekuwa akipita kando ya jengo hilo lilipoporomoka alisema kuwa alishtukia amefunikwa na vifusi ambavyo vilimuumiza mgongo.

“Niliumia kwenye mgongo wangu. Ninaomba Mungu anisaidie nipate nafuu,” alisema Bw Oreni.

Bi Kula Hache alisema kuwa walianza shughuli za uokoaji punde tu walipopokea ripoti hiyo. Pia aliwashukuru watu waliokuwa wakisaidia kuwaokoa waliokuwa wamekwama katika jumba hilo.
“Tunawashukuru watu ambao walikuja pamoja na kuanza kuwaokoa waliokuwa wamekwama vifusini na kuwaonya watu dhidi ya kujazana katika eneo hilo,” alisema Bi Hache.

Tukio hilo lilikatiza kwa muda mkutano wa magavana wawili na mbunge mmoja uliokuwa ukiendelea katika ofisi ya gavana Ongwae.

“Watu wanne wameaga dunia na wengine 39 wako hospitalini. Tutahakikisha kuwa wanaonusurika wanashughulikiwa kwa haraka,” akasema.

Kulingana na Bw Lucas Odera ambaye ni mkuu wa ujenzi NCA katika eneo la Nyanza, walikuwa wakiandaa ripoti kuhusu tukio hilo.

“Tunazidi kushughulikia jambo hilo na tutakapomaliza tutatoa ripoti yetu,” alisema.

Hata hivyo, afisa mmoja wa NCA ambaye aliomba kutotajwa alisema kuwa jengo hilo lilikuwa limeidhinishwa kujengwa hadi ghorofa tatu pekee.

“Tumekatiza ujenzi katika jengo hilo mara mbili kwa sababu mjenzi alikiuka sheria kwa kujenga ghorofa kumi badala ya tatu alivyoagizwa,” alisema afisa huyo.

Viongozi walioandamana na gavana Ongwae walielezea hisia zao kuhusiana na tukio hilo na kuwaomba wajenzi kuwa makini.

Gavana wa Nyamira Bw John Nyagarama alisema kuwa tukio hilo ni funzo kwa wajenzi ambao walikuwa wakijenga majumba katika mji huo.

“Tunawaomba wamiliki wa maghorofa ambayo yanajengwa kuhakikisha kuwa wanapata vibali kabla ya kuanza ujenzi,” alisema Bw Nyagarama.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako